Rais Samia ataka maboresho eneo kutunza watoto Kariakoo

By Pilly Kigome , Nipashe Jumapili
Published at 03:19 PM Feb 08 2026
Rais Samia Suluhu Hassan,
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan,

Rais Samia Suluhu Hassan, ameliagiza Shirika la Masoko Kariakoo, kutafuta wawekezaji wa kupata eneo la kulea watoto wachanga, ambao mama zao watakuwa wanafanya biashara katika soko kuu Kariakoo.

Ametoa maagizo hayo leo katika halfa ya uzinduzi wa Soko jipya la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Dk Samia amesema licha ya kuridhishwa na maboresho ya kuongeza vyumba maalum vya kunyonyeshea watoto wachanga, awali havikuwapo pia ameagiza kuongezwa kwa eneo maalum la kulelea watoto, ili mama zao wafanye biashara kwa weledi katika kujiongezea vipato vya familia.

"Hii italeta tija sokoni hapa kwa kuwa soko hili sasa linaangaliwa kimataifa zaidi na si kama ilivyokuwa awali" amesema.

Pia ameagiza kutolewe kwa mafunzo ya kutumia mitungi ya uzimaji moto, kwa wafanyabiashara wote sokoni hapo, ili yanapotokea majanga iwe rahisi kujihudumia na si kukimbia.