Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu amesema yupo tayari kuongoza mapambano ya kupigania demokrasia nchini kwa gharama yoyote kwa kushirikiana na vyama vingine.
Akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu cha chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hakainde Hichilema jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo amesema kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu mambo siyo rahisi hivyo kuahidi kushirikiana na vyma vingine ili kupigania demokrasia.
“Tukielekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni muhimu kutambua kwamba kuna hujuma na hila zinazotumiwa ili kukatisha tamaa wananchi.” Amesema Dorothy
“Hali hii inatufanya tuwe na jukumu kubwa la kusukuma ajenda ya kuunda jukwaa la mapambano ya pamoja na vyama makini. Tunahitaji kufanya shughuli za pamoja ili kuimarisha umoja wetu wenye nguvu utakao leta tija ya mabadiliko.” Amesema
“Tunahitaji kupambania kuurejesha uchaguzi huru. Nchi yetu hasa hakuna uchaguzi, tuna uchafuzi. Tutaunganisha nguvu na vyama vyote makini na wadau wa demokrasia nchini.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED