MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imetangaza mafanikio makubwa iliyoyapata katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Imetaja miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na serikali kuongeza uwekezaji katika ujenzi wa vyuo kutoka Sh. bilioni 116 hadi kufikia Sh. bilioni 516 hivi sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, alisema hayo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 30 ya utoaji na utekelezaji wa shughuli za mafunzo ya ufundi stadi nchini na miaka 50 ya utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi.
Kasore alisema ongezeko hilo la vyuo limesababisha kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kufikia 380,000 kutoka 38,360 waliokuwa wakidahiliwa mwaka 1994.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED