NDEGE iliyobeba abiria 181 imeanguka katika uwanja wa ndege kusini magharibi mwa Korea Kusini.
Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya asubuhi kwa majira ya huko, wakati ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan.
Picha zinaonekana ndege hiyo ikiteleza kutoka kwenye njia ya kurukia na kuangukia ukuta, kabla ya baadhi ya sehemu zake kuwaka moto.Shirika la Kitaifa la Zimamoto, limethibitisha kwamba watu 167 walifariki katika ajali hiyo ya ndege.
Awali, tulisikia pia kwamba wafanyikazi wawili wa ndege walipatikana wakiwa hai na kusafirishwa hadi hospitalini.Uwanja wa ndege wa Muan ni wa ukubwa wa kati, ulifunguliwa mwaka wa 2007 na una njia za kwenda nchi kadhaa za Asia.
Ajali hii si ya kawaida kwa Korea Kusini, ambayo imekuwa na rekodi nzuri ya usalama wa ndege katika miaka ya hivi karibuni.
Ikiwa idadi ya vifo itathibitishwa, hii itakuwa ajali mbaya zaidi ya ndege kuwahi kutokea katika ardhi ya Korea Kusini.
Inaonekana pia kuwa ajali mbaya pekee ambayo Jeju Air imepata katika historia yake ya karibu miaka 20.
Jeju Air ndilo shirika maarufu la ndege la bei nafuu nchini Korea Kusini, lenye safari nyingi za ndege katika eneo lote la Asia.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo alisema katika mkutano na wanahabari hapo awali shirika hilo la ndege halikuwa na historia ya ajali. Aliomba msamaha kwa familia za waathiriwa.
Chanzo: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED