Simba yaanika sababu kuwaacha Luis Miquissone, Kenedy Juma

By Faustine Feliciane ,, Adam Fungamwango , Nipashe
Published at 11:21 AM Jun 21 2024
 Luis Miquissone, Kenedy Juma.
Picha: Nipashe Digital
Luis Miquissone, Kenedy Juma.

UONGOZI wa klabu ya Simba kushuka kiwango na gharama kubwa ya mshahara ni sababu mojawapo ya kuamua kuachana na baadhi ya wachezaji wao kwenye kikosi hicho.

Inalezwa winga Luis Miquissone ni mchezaji aliyekuwa aklilipwa fedha nyingi kutokana na mkataba wake aliosaini wakati akirejea mara ya pili kwenye klabu hiyo akitokea Al Ahly ya Misri.

Mmoja wa viongozi ndani ya klabu hiyo aliiambia Nipashe kuwa, licha ya mshahara mkubwa aliokuwa akipokea, Miquissone hakuwa na mchango wowote ndani ya klabu hiyo akimaliza msimu bila kwenye Ligi Kuu.

"Simba ilikuwa inamlipa fedha nyingi za mshahara, lakini nadhani wanasimba wenye mashahidi, hata pale alipopewa nafasi hakuonyesha makali yake ambayo wanasimba wengi walikuwa na mategemeo naye," alisema kiongozi huyo na kuongeze, "Nikukumbushe tu Luis alirejea Simba Julai 22, mwaka jana akitokea Al Ahly, amecheza hapa kwa msimu mmoja tu, hakuwa na makali kama aliyoyaonyesha awali alipojiunga nasi, hajafunga bao lolote hadi msimu unamalizika, halafu ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi ndani ya kikosi, hii tumeona si sawa, tumeamua tuachana naye," alisema kiongozi huyo.

Mchezaji huyo, awali alijiunga na Simba 2020 na kucheza kwa msimu mmoja ambao ulikuwa na mafanikio makubwa, akiiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa, kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa akifunga baadhi ya mabao yaliyoiwezesha kufika hapo, ikiwemo kupachika bao pekee dhidi ya Al Ahly ya Misri, Februari 23, 2021.

Kiwango hicho kilimuwezesha kusajiliwa na Al Ahly, ambako hakuwa na wakati mzuri na kujikuta akirejea tena nchini msimu uliopita.

Alisema kwa upande wa Kenedy ni kiwango duni alichokionyesha huku akiwa na makosa mengi kwenye uchezaji ndio sababu ya kuachana naye na kumpa fursa ya kwenda sehemu nyingine kucheza.

Alisema bao la kujifunga la dakika ya 89 kwenye mchezo dhidi ya Namungo liliwakera viongozi na benchi la ufundi la klabu hiyo.

"Kenedy licha ya kupata nafasi ya mara kwa mara ya kucheza msimu uliomalika, kiwango chake hakikukuwa, amekuwa mchezaji wa kawaida na mwenye makosa mengi ndani ya uwanja, labda kama atapata timu nyingine atakuza kiwango chake," alisema Msemaji huyo.

Juzi jioni, Simba ilitoa taarifa ya kumuacha Kenedy na Miqussone na kuungana na Shaban Chilunda, John Bocco, Saido Ntibanzokiza kufikisha idadi ya wachezaji watano waliotangazwa kuachwa na timu hiyo.

Klabu hiyo kupitia kwa Menaja habari wake, Ahmed Ally alisema wataendelea kuwatangaza wachezaji wanaochana nao kabla ya kuanza kuwatangaza wale wanaowasajili kwa ajili ya msimu ujao