Kocha MC Alger: Licha ya joto kali, pointi 3 lazima

By Shufaa Lyimo , Nipashe
Published at 11:42 AM Jan 17 2025
Kocha Mkuu wa timu ya MC Alger, Khaled Benyahya.
Picha: Shufaa Lyimo
Kocha Mkuu wa timu ya MC Alger, Khaled Benyahya.

Kocha Mkuu wa timu ya MC Alger, Khaled Benyahya muda huu akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa kesho Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Yanga mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumzia mchezo huo amesema mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa.

"Mechi itakuwa na ushindani lakini tumejipanga vema kuhakikisha tunapata pointi tatu licha ya Dar kuwa na joto kali, amesema Ben Yahya.

Kwa upande wake Zakaria Draoui ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji amesema amejipanga vizuri kupata ushindi licha ya kuwepo na upinzani.

"Kwa upande wetu Tunafahamu ni mchezo ambao utakuwa na upinzani  hivyo lazima tuingie kwa tahadhari, amesema Draoui