Bendera ya Tanzania yapeperushwa vyema Nchini Rwanda

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:03 PM Jun 24 2024
Vyombo vya Usalama na Taasisi mbalimbali za Serikali ya  Tanzania kimekabidhi Bendera ya Taifa baada ya kurejea kutoka nchini Rwanda.
Picha: JWTZ
Vyombo vya Usalama na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania kimekabidhi Bendera ya Taifa baada ya kurejea kutoka nchini Rwanda.

Kikundi cha Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Vyombo vya Usalama na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania kimekabidhi Bendera ya Taifa baada ya kurejea kutoka nchini Rwanda.

Aidha kikundi hicho kilichoshiriki zoezi la 13 la Medani la Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki "FTX Ushirikiano Imara 2024" lililofanyika nchini Rwanda, kimekabidhi bendera hiyo mwishoni wa wiki iliyopita.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob  Mkunda, Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali, Iddi Nkambi  amewataka Maafisa na Askari walioshiriki zoezi hilo kutumia vizuri mafunzo waliyoipata kwenye zoezi hilo.

Alisema  wakati wanapotakiwa kukabiliana na matishio ya kiusalama na Majanga mbalimbali yanayoweza kutokea nchini, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

1
Naye Kamanda Kikosi cha JWTZ wa zoezi hilo Luteni Kanali, Benard Mongela amemshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda kwa kuwezesha kufanyika kwa zoezi hilo kwa kuwa washiriki wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu na wanajeshi wa EAC katika nyanja mbalimbali kama vile Ulinzi wa Amani, kukabiliana na matishio ya Ugaidi, Uharamia na Majanga ya kibinadamu.

Zoezi Ushirikiano Imara 2024 lilifanyika kuanzia Juni 6 hadi 23, mwaka huu.