KUTOKA katika kongamano la Mpango wa Taifa Kuzuia na Kudhibiti Magomjwa Yasiyoambukiza, lililofanyika Novemba, 2023, Meneja Mpango huo, Valeria Milinga, anasema kuna ongezeko la asilimia 9.4 kwa magonjwa yasiyoambukiza ikilinganishwa na miaka mitano ya nyuma.
Ikielezwa na matabibu wa magonjwa hayo, mufumo mbaya wa maisha ni sababu kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza, pia ulaji vyakula kiholea.
Dk. Mashili anafafanua kuwa, magojwa ya moyo pamoja na figo ndio ambayo yanaweza kwenda kuibua magonjwa mengine katika mwili wa binadamu, kutokana na kuchukuwa nafasi, pia ufanyaji kazi wake ni mkubwa.
Aidha anasema takwimu zinaonesha kwa mwaka Duniani asilimia 70 ya vifo vinatokana na magonjwa yasiyo ambukizwa, ikiwana Tanzania ni asilimia 34.4 kila mwaka watu hupoteza maisha huku chanzo ikiwa ni magonjwa yasiyo ambukizwa.
WANASHERIA NA YAO
Utumiaji bidhaa bila kuwa na lebo yenye kuonekana vizuri na kueleweka nma mchanganyiko wa vitu vya aina gani, vinasaidia nini katika kujenga afya ya mtumiaji, ikiwa sababu kubwa ya kumfanya mlaji kupata madhara kiafya.
Wadau wanadai kuwa, uwekaji wa lebo zenye rangi na zinazoinekana kwenye bidhaa mbalimbali, zinamfanya mlaji kuwa na uamuzi sahihi a kufahamu faida na hasara kiafya, ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa.
Vilevile wanahitaji maboresho hayo kwa wazalishaji wa bidhaa kuweka lebo kmbele ya kifungashio na zenye kuonesha vitu vilivyotumika katika uzalishaji kama vili sukari, chumvi na mafuta.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurungezi ya Chama cha Wanasherea Wanawake Tanzania (TAWLA), Wakili Vicencia Fuko, anasema vyakula vingi vilivyo pakiwa ndivyo huleta magonjwa yasiyoambukiza kwasbabu vimetengenezwa na chumvi, sukari pamoja na mafuta mabaya.
Pia anasema katika utengenezaji wake, utafiti unaonesha kuwa pindi vinapochakatwa vipo vitu vizuri hutolewa na vibaya vingi huongezwa, ili kumvutia mteja na kufanya ushindani wa viwanda ambavyo huzalisha bidhaa za kufanana.
Lengo ni kuwataka wazalishaji wa bidhaa za vyakula nchini, kuweka lebo zenye kuonesha rangi kama vile nyekundu, kijani na njano, ambazo zitamfanya mtumiaji kufanya uchaguzi sahihi ili kulinda afya yake.
Vilevile anaeleza namna bidhaa za asili zinavyoandaliwa kwa gharama, ukilinganisha na bidhaa zinazozalishwa viwandani, hiyo ndio sababu watu walio wengi wanashindwa kumudu vyakula vya asili na kujikuta wanatumia bidhaa ya ambazo tayari zimechakatwa viwandani.
Akifafanua Wakili huyo, inapaswa mlaji afanye maamuzi ya kutumia bidhaa, ambayo anafahamu faida na athali za matumizi yake, hivyo maboresho ya lebo katika bidhaa ni lazima iyonekane vizuri, iwe rahisi kueleweka pia ijirudie katika bidhaa.
Wakili na Maratibu wa Miradi wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Isabela Inchimbi, anasema kama chama wapo kwenye mradi wa kushawishi serikali kuwa na kanuni za lazima za viwango, ili kuhakikisha bidhaa zinazouzwa zinakuwa na taarifa kamili na kwa lugha nyepesi.
Hii ni kutokana na taarifa ya WHO kuwa vifo vitokanavyo na magonjwa yasio ambukizwa kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma, hivyo wanaamini kupitia uboreshaji wa kanuni itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa hao.
Vile vile Mratibu wa Kampeni ya Kemikali za Trans-fat Tanzania, Yosia Kimweli, anasema trans-fat, ina madhara kifya uthibitisho uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wanasayansi, kuwa inasababisha magonjwa ya moyo pamoja na mishipa ya damu.
Mfano wa vyakula hivyo keki, vidakuzi, mikate, bisibisi, pizza iliyogandishwa, biskuti, donati na kuku wa kukaanga, watu walio walio wengi wamejikuta wakitumia vitu hivyo ikiwa hawafahamu madhara ya kiafya kwa siku za mbeleni.
WHO inaishauri kiwango cha kemikali ya ‘transfat’ kiwe asilimia mbili, kwani kiwango zaidi ya hiyo kinasababisha hayo magonjwa, hivyo inahitajika kutungwa sheria kwa nchi za umoja wa mataifa kwani ni baadhi ambazo tayari zimeshatunga sheria kwa Afrika ni nchi mbili, za Afrika Kusini na Nigeria pekee.
Anasema kwa upende wa nchi za Afrika masahariki huna ambayo tayari imetunga sheria, ili kupunguza kiwango cha matumizi ya transfat kwenye bidhaa na kupunguza madhara hayo nchini.
Hivyo wakiwa kama Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, wanaiyomba selikari itunge sheria ya trans-fat, ili kulinda afya za watanzania pia kuendana na nchi wanachama wa umoja wa mataifa udhibiti majanga hayo nchini.
Lebo zenye kuonekana zitafanya mlaji kuwa na maamuzi sahihi, katika kuchagua chakula chenye kujenga mwili kiafya na hata kuepuka magonjwa yasiyoambukiza, ambayo husababishwa na vyakula hivyo.
SHERIA YENYEWE
Sheria ya Usalama wa Bidhaa za Watumiaji (CPSA), inasema lebo ya ufuatiliaji inapaswa kujumuisha mtengenezaji na mnunuzi, maelezo kama vile mahali na tarehe ya utengenezaji wa bidhaa, bechi, nambari ya uendeshaji au sifa zingine tambulishi na maelezo mengine yaliyoamuliwa na mtengenezaji, ili kusaidia kutambua chanzo mahususi cha bidhaa.
Taarifa zote za lebo ya ufuatiliaji lazima zionekane na kusomeka Kiambato kinapotambuliwa kuwa hatari au chanzo cha ukiukaji, lebo ya ufuatiliaji husaidia kutambua bidhaa zingine zilizo na kiungo sawa.
Sheria husika imo katika kifungu cha 14(a)(5) cha Sheria ya Usalama wa Bidhaa za Mtumiaji (CPSA), masharti haya hapo awali yalikuwa sehemu ya kifungu cha 103 cha Sheria ya Uboreshaji wa Usalama wa Bidhaa za Mtumiaji (CPSIA).
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED