Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo, amesema endapo itabainika mabomba ya sindano yaliyoonekana katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Azam Complex, yalitumika kwa ajili ya kuchoma sindano za kuongeza nguvu, timu husika itachukuliwa hatua.
Kasongo alisema ameona video hizo kupitia mitandao ya kijamii na kama ni suala la utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu ni haramu.
"Ni haramu kwa wachezaji, kwa viongozi ni haramu, kanuni zetu zinakataza wachezaji, zinakataza viongozi. Pale ambapo watapatikana na hatia, watafungiwa," alisema Kasongo.
Aliongeza bodi yake imelipokea na pale itakapobainika waliofanya walidhamiria kwa nia ovu, hatua zitachukuliwa.
"Kwa sasa hivi ni mapema mno, kwa sababu unaweza kukuta bomba la sindano, na sindano ina kazi nyingi, tumeona, na kuona kwetu imetupa mwanga kujua ni namna gani nzuri tutaliendelea bila kuleta madhara kwa vilabu ambao ndio tunafanya nao kazi, bila kuleta pia madhara kwa mashabiki wetu," aliongeza Kasongo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED