SHERIA ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ya mwaka 2010, ilianzisha vitengo viwili ambavyo ni Kitengo cha Uratibu wa PPP kilicho chini ya Wizara yenye dhamana ya Uwekezaji na Maendeleo ya Sekta Binafsi na Kitengo cha Fedha cha PPP kilicho chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Mwaka 2014, serikali ilifanyia marekebisho, kwa kuunganisha vitengo viwili vilivyoanzishwa awali na kuanzisha Kituo cha Ubia maarufu kama ‘One stop Center” chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwaka 2018 Sheria ya Kituo cha Ubia, ilifanyiwa marekebisho zaidi na kubadilisha majukumu ya mpango wa kituo hicho, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Wizara ya Fedha na Mipango.
Pia, Sera ya Ubia ilitungwa mwaka 2009 na Sheria ya Ubia ikafuata mwaka 2010, ili kutekeleza sera hiyo.
Hapo sheria nayo ikafanyiwa marekebisho kwa mara ya kwanza mwaka 2014 na mara ya pili mwaka 2018, mara ya tatu mwaka jana.
MALENGO YA KITUO
Hivyo Kituo cha Ubia, kilihamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu hadi Wizara ya Fedha na Mipango, ambako imeendelea kufanya kazi hadi leo, ikiwa na malengo yaliyopelekea kituo hicho kuanzishwa nchini.
Moja, ni kurahisisha uendelezaji na uratibu wa masuala yote yanayohusu utekelezaji wa programu ya PPP nchini; pia kufanya vibali kwa wakati na hivyo kupunguza muda wa usindikaji na kuondoa urudufu.
Vilevile, inatoa mwelekeo sahihi kwa mamlaka za ukandarasi na wawekezaji kupitia uundaji wa duka moja la kituo cha ubia na kuimarisha jukumu la usimamizi na usimamizi wa PPP, ili kuongeza kasi ya utekelezaji na maendeleo nchini.
Kwa sasa Kituo cha Ubia, kimeanza rasmi kufanya kazi, na David Kafulila akiwa ni Mkurungezi Mtendaji, anayeeleza namna ufanyaji kazi wao ulivyo ili kuhamasisha ubia kati ya serikali na sekta binafsi na kujenga uwezo kwa sekta binafsi.
Aidha, anataja suala la kujenga uwezo kwa mamlaka za serikali kujua namna gani wanaweza kushirikiana na sekta binafsi kwenye masuala ya ubia, hivyo kinachakata kupitia uchambuzi yakinifu zinazofanywa na pande zote mbili
INAVYOFANYA KAZI
Kafulila anafafanua namna ubia unaweza kuwa kwenye sekta mbalimbali, ikiwamo Maji, Afya, Elimu, Barabara, Viwanja vya Ndege, Bandari na zinginezo ambazo zinaweza kuingia kwenye ubia na kuleta maendeleo makubwa katika Taifa.
Hata hivyo, Kafulila anajigamba kuwa, Sheria ya Ubia Tanzania haijawahi kupitisha mkataba mbovu, kwa sababu sheria iko makini.
Vile vile anasema uwekezaji wa sekta binafsi unahitajika, ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya miundombinu kutokana na ongezeko la watu nchini na mahitaji ya huduma mbalimbali kuongezeka kwa wingi.
Mbinu hiyo anataja husaidia kuharakisha maendeleo na kuhakikisha huduma bora huku ikipunguza matatizo ya kifedha kwa serikali na kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wananchi kiurahisi, huku serikali ikiingiza kodi kutoka sekta husika.
Yapo manufaa ya kifedha anayotaja washirika wa kituo hicho kwa kutumia, fursa za kujenga ujuzi, jinsi namna mfumo wao thabiti wa kitaasisi na kisheria unavyosaidia utekelezaji wa PPP zilizofaulu na mada zinazofaa zaidi kama vile hadithi za mafanikio.
Anasema sekta binafsi inapoingia kwenye ubia na serikali katika kutekeleza mradi, ili kupata uwezo, uweledi namna ya kuendesha mradi husika, ndio maana tunaingia kwenye kutekeleza kwa muda tofauti kutokana na mradi husika.
Anataja inaweza kuchukua miaka mingi au kidogo kutegemea na hesabu za mradi husika zilivyo, yaani baada ya muda unaoweza kurudisha pesa na faida yake, ndipo aukabidhi mradi huo kwa serikali.
Kiongozi huyo anaeleza kuwa hadi kufikia sasa takribani miradi 74, ambayo ipo kwenye hatua mbalimbali za utambuzi kwenye sekta tofauti, mfano mradi wa barabara ya mwendo kasi Kibaha, Chalinze ambao kwa sasa upo kwenye hatua ya tathimini.
Aidha, anaeleza sifa kubwa ya sheria ya ubia Tanzania, ni yenye uwazi na yenye ubora inayoweza kuhakikisha maslahi ya umma na kampuni binafsi yanapatikana, yaani inaleta faida pande zote mbili.
Kafulila anasema, kuna umuhimu wa kubadilisha mtazamo wa umma kutumia ubia kufanya mradi wa serikali, ili kuepusha gharama kwa serikali ambazo zinaweza kufanywa na sekta binafsi, ili kudumisha miundombinu na huduma za umma zinazohitajika.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED