KAZI YA WATAFITI KIMATAIFA... Mambo 11 yanayoharibu ubongo kufanya kazi, kumbukumbu finyu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:12 AM Nov 07 2024
 Msongo wa mawazo unatajwa kuchangia madhara ya ubongo na kumbukumbu.
Picha: Mtandao
Msongo wa mawazo unatajwa kuchangia madhara ya ubongo na kumbukumbu.

SHULE ya Kitabibu ya Harvard, ambayo ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Havard, wakishirikiana na Taasisi ya Kitaifa ya Marekani ya Magonjwa ya Mifumo ya Mishipa, pia Shinikizo zimetafiti na kuja na majibu yafuatayo.

Hapo, imeorodhesha mambo 11 katika ubongo wa binadamu, ambayo yanapopewa nafasi huweza kuleta athari, kama vile hali ya kuwa na usahaulifu. 

Mosi, ni kukosa usingizi unaotosha: Kwa mujibu wa Kituo cha Sayansi ya mfumo wa neva (Neurology) cha Marekani, uharibifu mkubwa wa ubongo unasababishwa na kutokuwa na usingizi wa kutosha. 

Usingizi wa kutosha kwa watu wazima unamaanisha ni saa saba hadi nane, kati ya saa 24 kwa siku. Wataalamu wanasema kulala mfululizo usiku ni bora zaidi, kwani ubongo unapumzika na kuunda seli mpya wakati wa kulala kwa saa saba na zaidi. 

Ili kufanya hivyo, mtu anahitaji wakati anajiandaa kwenda kulala angalau saa moja kabla, asitumie kifaa chochote wakati huo, anasafisha chumba chake na uso usifunikiwe anapolala, kwani kunadhibiti mwenendo wa kutumia hewa ya Oksijeni mwilini. 

Pili, kifungua kinywa: Hicho ndicho kinachotoa nishati ya kufanya kazi siku nzima. Kutotumia huko kunapunguza viwango vya sukari kwenye damu, hata kuathiri uwezo wa ubongo.

 Tatu, kutokunywa maji ya kutosha: Asimilia 75 ya ubongo ni maji. Hivyo, kuiweka katika hali ya unyevu ni muhimu kwa utendaji wake. Ukosefu wa maji husababisha tishu za ubongo kupungua na seli kupoteza kazi. 

Wataalamu wanashauri mtu mzima anapaswa kunywa walau lita mbili za maji kwa siku. 

Nne, ni msongo wa mawazo uliozidi: Kuwa na hali hiyo kwa muda mrefu, husababisha seli za ubongo kufa na sehemu ya mbele ya ubongo kusinyaa, ikiathiri kumbukumbu na uwezo wa kufikiria. 

Jamii inashauriwa kuepuka majukumu ya ziada kadri inavyowezekana. 

Tano, matumizi ‘vikokotoo’ kupita kiasi: Katika kazi za mahesabu madogo, yanafaa kufanyika bila ya kutumia vikokotoo. Kusoma vitabu na yanayofanana na hayo, kunatajwa kuimarisha ujuzi wa akili ya binadamu. 

Tabia hizo zinatajwa kuwa mazoezi ya ubongo, ambayo huweka nguvu zake za kufikiri na kumbukumbu imara kwa muda mrefu. 

Kando na hiyo, mtu anaweza kucheza michezo tofauti ya shughuli za ubongo, kama kucheza ujumbe wa maneno, kulinganisha mafumbo. 

Sita, kutumia vipokea sauti kila wakati, pia kusikiliza muziki wa sauti kubwa: Sauti inayoingia masikioni kwa vinavyobanwa kichwani zina madhara. 

Pia, kusikiliza kwa sauti kubwa au kwa muda mrefu kwa kelele kubwa, nako kunasababisha atahari.

Mtu uwezo wake wa kusikiliza unapoathrika, unatajwa hakurekebishiki na inakuwa na amdhara hata katika kazi ya ubongo na kumbukumbu. 

Kunashauriwa, mtu anaposikiliza nyimbo kwa kutumia vipokea sauti masikioni kwa muda mrefu, asiongeze sauti zaidi ya asilimia 60.  Pia, asisikilize mfululizo, ajipe mapumziko walau kwa saa moja. 

Saba, kuna mtazamo wa mtu kukaa pekee muda mrefu, hachangamani na wengine: Kuzungumza na watu kunatajwa muhimu kwa afya ya ubongo na kutumia muda mrefu uko pekeee ni mbaya kwa ubongo wako, sawa na kutopata usingizi wa kutosha.

 Mjumuiko na marafiki na familia huweka akili safi. Upweke unatajwa kuongeza hatari ya wasiwasi na shida ya akili. 

Kuweka ubongo wako kuwa na afya, mtu anatakiwa kujumuika na marafiki wa karibu au wanamilia kila mara, ila wawe wenye mawazo chanya kimaisha. 

Nane, kutawaliwa na mawazo hasi: Mtu anapokuwa na tabia ya kuwaza mambo hasi kila wakati, humuwekea mwelekeo wa giza aendako na hata akaangukia hatari kwa afya ya ubongo wake. 

Hiyo ni kwa sababu mawazo mabaya, huunda msongo wa mawazo, pia wasiwasi wakati wote, hali inayojilimbikiza ubongo, ambako ndiko kwenye hazina ya kubukumbu. 

Mtu anashauriwa kuacha mawazo mabaya anayodumu nayo muda mrefu, kwani inamhatarisha kuwa na tabia aina hiyo. Ikiwa mtu hawezi kubadilika peke yake, anashauriwa kutafuta msaada wa daktari wa akili. 

Suala la kuepuka urafiki mbaya unatajwa ni muhimu, hali kadhalika, kuwa karibu au kufuatilia habari mbaya. 

Tisa, mtu kuwa na muda mrefu gizani: Utafiti nchini Marekani, umeonyesha kuwa watu wanaotumia muda mrefu gizani au wanatumia muda mrefu katika maeneo yaliyofungwa na hakuna mwanga wa kutosha, pia mzunguko wa hewa, ni mazingira yanawasogeza kwenye shinikizo la ubongo. 

Hiyo ni kwa sababu yatokanayo na mwanga wa jua ni muhimu sana kwa ubongo na kufanikisha hilo, mtu anaaswa kupata muda wa kuwapo juani kila siku. Mathalan, nyumbani anaungua milango na madirisha hewa safi na mwanga wa unamfikia. 

Kumi, ni kula kula kupita kiasi: Haijalishi aina ya chakula iwe cha afya, au la. Kula kupita kiasi kunaharibu ubongo wa mtu na utafiti unaweka bayana kwamba, ulaji unaopitiliza huziba mishipa ya ubongo na kupunguza mtiririko wa damu. 

Hiyo husababisha kupoteza kumbukumbu na kufikiri na shida inafika kwenye akili yake.

Sambamba na hilo, kuna la kula vyakula visivyofaa hasa vya kukaanga, vyenye sukari nyingi zaidi, pia vinywaji baridi, inanagukia hatari kwa ubongo. 

Hapo ndiyo inapobeba ujumbe wa umuhimu kuwa na chakula cha wastani na sahihi. Inaelezwa na wataalamu kwamba watu wengi wanadhani kuwa lishe inaishia kuondoa mafuta.  

Lakini ukweli unabaki kwamba, asilimia 60 ya ubongo wa binadamu ni mafuta na kila aina ya chakula kinapaswa kuliwa, katika kuujenga, ‘kigezo na mashati’ vyakula vinapaswa kuliwa kwa kiasi kinachofaa. 

Hata hivyo, tahadhari kuu inaangukia hoja kwamba unywaji pombe na uvutaji sigara nao ni hatari kwa afya ya ubongo. 

Zinatajwa kuwa na tabia ya kubana mishipa ya fahamu ya ubongo na kuharibu seli na kwa hiyo, eneo la ubongo ambayo ndiyo kumbukumbu inahifadhiwa, haiwezi kukua. 

Mwisho, ni kwamba: Watu wanapotumia ‘skrini’ kwa muda mrefu inatajwa ni kifaa chenye athari kubwa kwa ukubwa na ukuaji wa ubongo.  

Pia, utumiaji simu za mkononi kwa Watoto, unatajwa kusababisha uharibifu zaidi kwenye gamba la mbele ya ubongo. 

Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanaotumia simu zaidi ya saa saba kwa siku wanadhurika. Kwa sababu, kukaa muda mrefu kwenye simu za mkononi kunasababisha shida kama maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa na uvimbe wa ubongo. 

Kwa sababu hiyo, ‘skrini’ wanayotumia watoto inapaswa kuboreshwa. Pia, watu wanashauria wasilale na simu karibu na mwili. 

Vilevile, simu inatajwa inafaa kuwekwa kwenye begi badala ya mfukoni. Mtu akiwa anataka kuzungumza kwa muda mrefu, afanyue hivyo kupitia spika, bila kushikilia simu sikioni na kutuma ujumbe wa maandishi, inatajwa ni mbadlka bora kuliko kuzungumza. 

·    Kwa mujibu wa BBC