Watanzania 301 wasio raia Marekani kurudishwa nchini

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 05:57 PM Jan 28 2025
Rais wa Marekani Donald
Picha ; Mtandao
Rais wa Marekani Donald

MAREKANI kupitia Idara ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE) pamoja na Operesheni ya Utekelezaji na Undoaji (ERO), imesema kuanzia Novemba mwaka jana, watu 1,445,549 kati yao Watanzania 301 ambao si raia wataondoshwa nchi humo.

Miongoni mwa raia wanaoondoshwa nchini humo kutoka nchi 108, wamo kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) 8,946 kinara akiwa Somalia akiwa na raia wengi ambao ni 4,090 kati ya hao.

Trump akiwa na mkewe siku alipoapishwa
Taarifa ya ICE imebainisha hayo leo, kwamba taasisi hiyo ina wajibu wa kuwaondoa watu wasio raia na ambao hawana nyaraka zozote kisheria.