VIJANA wapatao 50 wanaojifunza maswala ya umeme katika Chuo cha Utundi Stadi (VETA) Wilaya ya Mkinga wameanza kuwa msaada mkubwa kwa jamii inayowazunguka wilayani humo.
Vijana hao wamekuwa wakisaidia shughuli mbalimbali ikiwemo ya kuwaunganishia wananchi umeme bila tozo ni kama kurudisha fadhila kwa wananchi hao.
Hayo yamesemwa kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Gilbert Kalima na Ofisa Tarafa ya Mkinga Heugen Mkinga kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Ufundi Stadi na miaka 30 ya VETA katika viwanja vya chuo hicho.
"Ndugu zangu, kwa Mkinga vijiji 85 vimeshasambaziwa umeme bado vitongoji, ni imani yangu wale vijana 50 wanaosomeshwa hapa kuwasaidia wananchi na kutatua kero walizokuwa wanazipata,
"Awali kabla chuo hiki hakijajengwa hapa tulikuwa tunaeafuata mafunfi umeme kutoka Wilaya ya Tanga, lakini tuna imani wananchi watakwenda kuipata huduma ile kwa karibu na kwa wakati" amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED