RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuwa amefanya mazungumzo ya tija na Katibu wa Marekani Marco Rubio na kuelewana kuhusu hitaji la kuhakikisha kusitishwa kwa mapigani katika DRC Mashariki.
Kagame ameeleza hayo katika mtandao wake wa X(Twitter) na kutaja miongoni mwa mazungumzo yao kuwa ni pamoja na kushughulikia sababu za msingi za mzozo mara moja na kwa uhakika.
“Pamoja na umuhimu wa kuimarisha uhusiano wetu karibu na kulingana na heshima kwa maslahi yetu ya kitaifa. Natarajia kushirikiana na Utawala wa Trump kuunda ustawi na usalama ambao watu wa eneo letu wanastahili,” ameandika Kagame.
Katika hatua nyingine Rais wa Kenya Willium Ruto, amekiri pia kufanya mazungumzo ya simu na Katibu wa Marekani, Marco Rubio, kuhusu hali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mashariki na msaada unaohitajika kutoka Marekani.
“Nilimpa Katibu Rubio taarifa kuhusu hali ya usalama nchini Sudan, Sudan Kusini, na Somalia. Ni furaha yangu kwamba Marekani imejikita kuendelea kutumia uwezo wake kusaidia ujumbe wa amani wa Kenya katika eneo hili,” aliandika Ruto.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED