KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewaonya wana CCM ambao wameanza kufanya kampeni chafu za kuwachafua wabunge walioko madarakani katika maeneo mbalimbali nchini.
Dk. Nchimbi, alitoa onyo hilo leo jijini Dodoma, wakati akifungua mafunzo kwa makatibu Kata na Matawi wa chama hicho, Wilaya ya Dodoma.
Alisema, hivi sasa kumeibuka tabia kwa baadhi ya wanachama hicho, kuanza kufanya kampeni chafu za kuwachafua wabunge walioko madarakani, ikiwamo kuchapisha T shirt kwa ajili ya kuwachafua.
“Kumeibuka tabia ya wana CCM ambao wameanza kampeni chafu za kuchafua wenzao, wapo ambao wanachapisha hadi T shirt ambazo zimeandikwa maneno ya kashfa kwa wale walioko madarakani,” alisema.
Hata hivyo alisema katika uchaguzi mkuu mwaka huu, CCM haitowapitisha wanachama wa aina hiyo, kuwa wagombea katika uchaguzi huo, bali majina yao yatakatwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED