Londo aapishwa Ubunge Afrika Mashariki

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:23 PM Oct 24 2024
Londo aapishwa Ubunge Afrika Mashariki
Picha:Mtandao
Londo aapishwa Ubunge Afrika Mashariki

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa kwanza wa Mkutano wa tatu wa Bunge la tano uliofanyika Kampala Uganda.

Katika mkutano huo, amesindikizwa na wajumbe wengine wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), kutoka nchini akiwamo Abdullah Makame, walioshuhudia hatua hiyo.

Uteuzi wake unaongeza uwakilishi wa Tanzania katika EALA, ambayo ina jukumu muhimu katika kuongoza mchakato wa mshikamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akihutubia baada ya kuapishwa Londo amesema "Hii ni mara yangu ya kwanza kujitokeza mbele ya Bunge hili ninapenda kuchukua nafasi hii kuahidi kujitolea kwangu na dhamira yangu isiyoyumba katika ajenda ya mtangamano wa EAC."

Londo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda kwamba utaongeza uzalishaji mali, kuboresha hali ya maisha, na kuongeza ushindani katika Jukwaa la Kimataifa.

Amehitimisha hotuba akisistiza dhamira yake ni kufanya kazi kwa karibu na wanachama wenzake wa EALA ili kujenga eneo lenye nguvu na ustawi zaidi.

"Ninapohitimisha, ninawashukuru kwa mara nyingine tena kwa kunikumbatia katika familia hii kwa pamoja tutashiriki, kuvumilia, na kufanya maboresho makubwa katika eneo letu" amesema.