WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii jinsia Wanawake na Makundil Maalumu Dk. Dorothy Gwajima amewataka wazazi kujenga utamaduni wa kuandika mirathi ili kuepusha migogoro ya kifamilia dhidi ya watoto wao pindi wanapofariki.
"Ndugu zangu wanaume kwa dhati ya moyo wangu hasa nyie wanaume niliyoyasikia na kuyashuhudia katika kuhudumu kwenye hii wizara, kama umeoa na kama una watoto hata kama hujaoa naomba andikeni mirathi yenu mapema kabisa Ili mkitangulia au akitangulia mbela ya haki mmoja wenu msiache watoto kwenye mitihani.
"Tunapata mitihani sana kwenye hizi kesi mtakuja kukumbuka huu wosia. Dunia imeshajaa hila, fitna, husda na tamaa za mali ambazo mtu hazimuhusu na umdhaniaye siye anakuja kuwa yeye kabisa.
"Watoto wadogo wanaumia mzazi aliyebaki na mtoto anaumia ni vilio mara nyingi na wanawake na watoto ndio wanaumia hapa" aliandika Gwajima kupitia mtandao wake wa kijamii.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED