KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali za upandaji miti kwa lengo la utunzaji wa mazingira, kampuni ya Jubilee Insurance Tanzania, ikishirikiana na wanafunzi na walimu, imeshiriki katika upandaji miti zaidi ya 400 katika shule mbili mkoani Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo zoezi hilo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam, katika Shule ya Msingi Mikumi na Mzimuni, ambako zaidi ya miti 200 imepandwa katika kila shule.
Imeeleza kuwa hatua hiyo ni katika jitihada za kurudisha fadhila kwa jamii kupitia kampeni yeo ya (Net Zero) ambayo imeanzishwa mahususi kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti.
"Lengo ni kupaanda miti tofauti kama vile ya matunda, ya madawa na ya vivuli. Hii ni ili kuboresha mazingira na kuwapa wanafunzi hamasa ya kuendelea kushiriki vyema katika masomo yao haswa yale yanayohusiana na mazingira," imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Imeongeza kuwa malengo ya kampeni hiyo ni kuendelea kufikia shule katika maeneo mbalimbali ndabi na nje ya mkoa huo, na kwamba hadi sasa wameshapanda miti zaidi ya 600 katika shule tatu.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED