DC Mbozi afariki dunia, Rais Samia ‘amlilia’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:46 PM Jan 14 2025
DC Mbozi afariki dunia,  Rais Samia ‘amlilia’.
Picha: Mtandao
DC Mbozi afariki dunia, Rais Samia ‘amlilia’.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Ester Mahawe amefariki dunia leo Januari 14, 2024 wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.

Kupitia mitandao ya kijamii , Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameandika ujumbe ufuatao:

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro. 

Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji. "

Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. 

Amina.


1