Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga leo Februari 14, 2025 amemuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dk. Doto Biteko kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuia ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.
Baraza la kisekta limekutana kujadili miradi ambayo inatekelezwa ambayo ni pamoja na mradi wa kufua umeme wa Nsongezi utakaotekelezwa na Nchi za Tanzania, Rwanda na Uganda ambapo Mawaziri husika watasaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji wa Mradi huu.
Aidha, Baraza hili linasimamia Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo litafanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 Jijini, Dar es Salaam.
Uenyeji wa Tanzania katika kongamano hilo unatokana na maamuzi ya mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta lililofanyika Mwezi Februari 2024 ambalo liliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano hilo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED