Elon Musk: USAID linapaswa kuvunjwa, ni shirika la kiuhalifu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:57 AM Feb 03 2025
Elon Musk: USAID linapaswa kuvunjwa, ni shirika la kiuhalifu.
Picha: Mtandao
Elon Musk: USAID linapaswa kuvunjwa, ni shirika la kiuhalifu.

Mmiliki wa kampuni ya teknolojia ya Tesla na SpaceX, Elon Musk, ametangaza kuwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) linapaswa kuvunjwa kwa kuwa ni shirika la kiuhalifu.

Musk, ambaye aliteuliwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), alitoa kauli hiyo baada ya maafisa wawili wa USAID kujaribu kuwazuia wafanyakazi wa idara yake kupata ufikiaji wa mifumo ya usalama ya shirika hilo.

Madai haya yamezua mjadala mpana kuhusu nafasi ya USAID katika masuala ya usalama na ufanisi wa serikali. Hadi sasa, USAID haijatoa tamko rasmi kuhusiana na tuhuma hizo.