WANAFUNZI 30 wa shule ya St Mary’s Mbezi waliopata daraja la kwanza kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka huu wamepewa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu.
Hafla ya kuwapa zawadi wanafunzi hao ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo na kushuhudiwa na wazazi wa wanafunzi hao walimu na uongozi wa shule za St Mary’s.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa shule ya sekondari Mbezi, Reca Ntipoo alisema kwenye mtihani wa kidato cha nne wanafunzi 30 wa shule hiyo walipata daraja la kwanza, wanafunzi 66 daraja la pili na wanafunzi 42 walipata daraja la tatu.
“Tofauti yetu na shule zingine ni kwamba sisi hatuchukui wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana tunachukua wanafunzi bila kubagua uwezo wao darasani tunawafundisha mpaka wanapata daraja la kwanza au la pili,” alisema
“Kwa hiyo tuliposajili wanafunzi wengi baadhi ya viongozi waliogopa lakini tuliwaambia msiwe na wasiwasi walimu wetu wako vizuri sana watafaulu na leo hii najisikia fahari kuona kweli wamefanya vizuri wote,” alisema
Alisema siri ya mafanikio ya shule hiyo ni ari ya walimu kutimiza wajibu wao kutokana na mazingira mazuri ambayo uongozi wa shule hizo umewawekea shuleni hapo.
“ St Marys tumeendelea kupanda kitaaluma mwaka hadi mwaka na siri kubwa ni mazingira mazuri ya shule ambayo wawekezaji wameweka ya kujifunzia, tuna maktaba na maabara nzuri sana ndiyo maana kwenye masomo ya sayansi wanafunzi karibu wote wamepata alama A,” alisema
“Viongozi wamekuwa wasikivu sana kwa changamoto yoyote inayotokea na leo wamewaandalia zawadi wanafunzi waliopata daraja la kwanza tumewapa zawadi pamoja na walimu zikiwemo fedha taslim,” alisema
Aliwahamasisha wazazi kuwaleta watoto wao shule za St Marys kwani ni sehemu nzuri sana kuwaea waoto kwasababu wanalelewa kiroho na kitaaluma na walimu wanajituma sana kufundisha usiku na mchana.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED