Uuzwaji tiketi za Pamba Day wazinduliwa rasmi

By Neema Emmanuel , Nipashe
Published at 07:16 PM Jul 22 2024
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizindua uuzaji wa tiketi kwa ajili ya tamasha la Pamba Day.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizindua uuzaji wa tiketi kwa ajili ya tamasha la Pamba Day.

UUZWAJI wa tiketi za kuingilia katika tamasha la Pamba Day Agosti 10 mwaka huu wazinduliwa rasmi huku wapenzi,wadau na wananchi wakiaswa kununua mapema tiketi ili kiwahi nafasi.

Akizindua uuzwaji wa tiketi hizo katika Uwanja wa Nyamagana,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ,amesema tiketi hizo zitatumika kuingilia uwanjani kushuhudia tamasha hilo.

" Tamasha la Pamba Day linatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, Agosti 10 mwaka huu,zimetengenezwa tiketi 25,000 na kuwataka washabiki na wananchi kuwahi kununua tiketi kabla nafasi hazijaisha ili kujiona na kupata raha waliyoikosa kwa miaka 23.

Amesema  leo ni siku ya uzinduzi na mkutano wa wadau kutoa maoni kuhusu Pamba Jiji pia serikali ikishirikiana na uongozi wa Pamba Jiji imedhamiria kurejesha heshima ya Mwanza katika soka na furaha ya mashabiki wa timu hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda akizindua uuzaji wa tiketi kwa ajili ya tamasha la Pamba Day.


Mtanda amesema Pamba Jiji ni mali ya wadau kila mmoja ana haki ya kuipigania hata kwa matambiko na maombi ili timu ifanye vizuri, hivyo waipe ushirikiano wa kutosha.

"Siku ya Pamba (Pamba Day) tutakuwa na wasanii mbalimbali watatumbuiza akiwemo Fid Q na Harmonize mpaka sasa zaidi ya tiketi 5300 zimeuzwa , kutakuwa na tiketi za sh.100,000 kwa jukwaa la V-VIP, Sh.50,000 kwa VIP,sh.10,000 na sh. 3000 mzunguko"anaeleza.