Chama cha soka cha England, FA, leo asubuhi kimetangaza kwamba, Thomas Tuchel amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England hadi mwaka 2028, kwa mujibu wa gazeri la Daily Mail.
Mkataba wa sasa wa Tuchel ambaye ni raia wa Ujerumani ulitarajiwa kumalizika baada ya Kombe la Dunia litakalofanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, mwaka huu.
Maofisa wa FA wamechukua hatua ya kumuongezea mktaba huo, baada ya kampeni ya kuvutia ya kufuzu michuano hiyo, huku kukiwa na wasiwasi kwamba, Tuchel anaweza kuwa kwenye rada za kutakiwa kuinoa Klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu huu.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED