Transit, Geita Gold kibaruani

By Adam Fungamwango , Nipashe
Published at 07:41 AM Oct 04 2024
Transit Camp
Picha:Mtandao
Transit Camp

RAUNDI ya tatu ya Ligi ya Championship inaendelea leo Maafande wa Transit Camp kuwakaribisha Geita Gold, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Maafande hao hawajashinda mchezo wowote kati michezo miwili iliyocheza Geita Gold nayo ikiwa haijashinda, lakini imetoa sare michezo yote miwili.

African Sports itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro ikiikaribisha  Pwani,, ambayo imeonekana kuwa tishio kwenye ligi hiyo.

Vigogo hao wa Tanga, Africans Sports nao hawajashinda mchezo wowote, ikitoka sare moja na kupoteza mmoja, inacheza na Songea United, ambayo imeshinda michezo yake yote miwili na kushika nafasi ya pili ya msimamo, ikiwa na pointi sita.

Mechi nyingine itakayopigwa leo ni kati ya Kiluvya FC ya Pwani, ambayo itashuka Uwanja wa Mabatini, Mlandizi kucheza dhidi ya Polisi Tanzania.

Kiluvya, ambayo ni mara ya kwanza kucheza Ligi ya Champioship ikitoka 'first league', imepoteza michezo yote miwili ambayo imeshacheza sawa na Polisi Tanzania iliyoshuka kutoka Ligi Kuu Bara msimu uliopita.