‎Simba SC yasonga mbele, KMC yatupwa nje FA Cup ‎

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:18 PM Feb 17 2026
‎Simba SC yasonga mbele, KMC yatupwa nje FA Cup
‎
Picha: Mpigapicha Wetu
‎Simba SC yasonga mbele, KMC yatupwa nje FA Cup ‎

‎Mnyama ametinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya Kombe la FA baada ya kuifunga Greenland FC kutoka mkoani Kagera mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, Dar es Salaam leo.

‎Wekundu wa Msimbazi walienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

‎Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Baraka Mwangosi, Antony Mligo na Neo Maema.

‎KMC FC imetolewa katika mashindano hayo baada ya kukubali kufungwa penalti 3-2 na Bandari Tanzania kutoka mkoani, Mtwara.

‎Timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 3-3, mechi ikichezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.

‎Fountain Gate pia imesonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuifunga Mapinduzi bao 1-0 huku Coastal Union ikiwaondoa Nyumbu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 wakati Biashara United ya Mara wakishindwa kufika uwanjani kuwakabili Mbeya City ya Mbeya.

‎Hatua ya 64 bora ya mashindano hayo itamalizika kesho kwa michezo 18 kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini, ambapo mabingwa watetezi, Yanga watawakaribisha Cosmopolitan ya Dar es Salaam.

‎Bingwa wa mashindano hayo hupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.