Gamond apewa miaka miwili kuinoa Stars

By Shufaa Lyimo , Nipashe
Published at 12:39 PM Feb 16 2026
news
Picha Mtandao
Gamond apewa miaka miwili kuinoa Stars

WIZARA ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imemtangaza rasmi Miguel Gamond kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Paul Makonda, amesema Gamond amepewa mkabata huo baada ya serikali kuridhishwa na kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi kifupi alichokuwa amekabidhiwa timu hiyo.

1
"Serikali imeamua kumpa Gamond jukumu la kuionoa timu yetu ya Taifa kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha muda mfupi alipokuwa amekabidhiwa timu hiyo," amesema Makonda. 

Amesema kocha huyo amekuwa miongoni mwa makocha bora ambao anaamini kupitia uwezo wake dunia nzima itaitambua Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi kubwa anazozifanya katika michezo.

Naye, Miguel Gamond ameishukuru serikali pamoja na shirikisho hilo kwa kumuamini, akisema atafanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuifikisha mbali timu ya Taifa.

2