Nchi 56 kushiriki Kili Marathon Moshi

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 05:23 PM Jan 18 2025
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Chisseo Nzowa akizungumza jana jioni, kabla ya kuzindua maandalizj ya mbio hizo za Februari 23 mwaka huu.
Picha: Godfrey Mushi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Chisseo Nzowa akizungumza jana jioni, kabla ya kuzindua maandalizj ya mbio hizo za Februari 23 mwaka huu.

MBIO za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon maarufu Kili Marathon, ambazo zitafanyika Februari 23 mwaka huu, zimezinduliwa rasmi katika Mji wa Moshi, huku serikali ikisema inajiandaa kupokea ugeni wa watu 12,000.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, aliyewakilishwa na Katibu Tawala Mkoa huo, Chisseo Nzowa, amesema mashindano hayo ya kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, yanawaleta pamoja watu kutoka takribani nchi 56.

“Mbali na kukuza afya ya watu na kukuza michezo, mbio hizi ambazo sasa ni maarufu Barani Afrika, pia zinachangia kukuza uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla; kupitia sekta ya utalii kila mwaka.

 

“Hii ni kutokana na washiriki wa ngazi zote wanaokuweko mkoani Kilimanjaro kipindi chote cha mbio hizo. Tunajivunia mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon, ambazo zimeendelea kuwa maarufu kila mwaka

 

…Tukio hili kwa sasa, limekuwa maarufu huku likiwashirikisha zaidi ya watu 12,000 na idadi kama hiyo ya mashabiki wanaokuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kulifuatilia.”

 

Mkuu huyo wa Mkoa, ametoa rai kwa wadau wote wa michezo kushirikiana kwa karibu na waandaaji wa mbio hizo ili ziendelee kuleta manufaa zaidi ya kiuchumi kwa mkoa, taifa na kwa mtu mmoja mmoja kutokana na ukweli kwamba mashindano hayo yanazidi kukua na sambamba na umaarufu wake kuendelea kukua kila mwaka.

 

"Mbio hizi huandaliwa kila mwaka, na mwaka huu ni msimu wake wa 23, manafuaa yake kiuchumi yanaonekana wazi kwa jamii yote ya Watanzania, kutokana pamoja na mambo mengine kukua kwa biashara mbalimbali hususan katika mji wa Moshi; nitoe wito kwa wafanyabiashara wote wa Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro, kuhakikisha wanazingatia ubora katika kutoa huduma zao ili kulinda heshima ya Mkoa katika nyanja za kibiashara.

 

Zaidi aliongeza, “Nichukue fursa hii kuwapongeza wadhamini wote wa mbio hizi wakiongozwa na mdhamini mkuu Kilimanjaro Premium Lager ambao wanadhamini mbio za kilomita, kampuni ya YAS ambao wanadhamini mbio za kilomita 21 (Yas Half Marathon) pamoja na Benki ya CRDB ambao wanadhamini mbio za kilomita 5.

 

“Napenda pia kuwaponegza wadhamini wengine ambao wanaunga mkono mbio hizo ambao ni pamoja na kampuni ya saruji ya Simba (Simba Cement), Kilimanjaro Water, TotalEnergies, kampuni ya TPC Sugar Ltd, Wasambazaji rasmi GardaWorld, CMC Automobiles, Salinero- Kilimanjaro, Kibo Palace Hotel na Keys Hotel, ambao ushiriki wao umechangia kuendelea kukua kwa mbio hizi.”

 

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Khensani Mkhombo, akizungumzia kuhusu zawadi zilizoandaliwa kwa msimu wa 2025, amesema kuwa Kilimanjaro Premium Lager, imetenga jumla ya Sh. milioni 30.

Washindi wa kilomita 42 kwa wanaume na wanawake kila mmoja anatarajiwa kupata zawadi ya Sh. milioni 5.5, ambapo wanariadha wa Kitanzania, watakaoshika nafasi ya kwanza katika mbio za kilomita 42 watapata bakshishi ya 550,000 kila mmoja.

Mkurugenzi huyo, amesema udhamini huo unalenga kuboresha Maisha ya watu pamoja na sekta ya michezo, pia umelenga kukuza uchumi wa taifa kupitia sekta ya utalii.

 

“Kutokana na mbio hizi kuzidi kupata umaarufu, mwaka huu, kamati ya maandalizi ya mbio hizi imekuja na mkakati mpya unaolenga kufanya matamasha ya utangulizi ambayo yatakayofanyika siku za mwisho wa wiki kuelekea mbio hizi, amapo matamasha hayo yataanza Ijumaa na kumalizika Jumapili, ambayo ndiyo siku ya mbio hizo”, amesema.

 

Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Biashara YAS, Isack Nchunda amesema, "Mwaka huu tunaadhimisha na kujivunia kuwa sehemu ya udhamini wa mbio hizi maarufu Barani Afrika kwa muongo wa kumi sasa, kupitia udhamini wetu wa mbio za kilomita 21 maarufu kama Yas Half Marathon. Kitengo hiki kinawaleta washiriki takribani 6,500, wakiwemo wanariadha maarufu Barani Afrika”.

 

Amesema mwaka huu, wakimbiaji na washiriki wengine wa pembeni kwa maana ya mashabiki wa mbio hizo watarajie kuona mambo mazuri kwenye mbio za kilomita 21 kutokana na uzoefu walionao wadhamini wambio hizo ambao ni Yas, akitoa rai kwa washiriki wa mbio hizo kujitokeza mapeam kuwahi nafasi zao kabla mbio hizo hazijaanza siku ya tukio hilo.



Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, David Peter, amesema kampuni hiyo inajivunia kuwa mmoja wa washiriki wa Karibu wa mbio hizo maarufu kupitia udhamini wake katika mbio za kilomita 5 za mashindano ya Kilimanjaro Marathon.

 

“Kwetu hili ni jukwaa sahihi la kuitangaza benki yetu kwani tunatarajia kuwafikia Watanzania wengi wa Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wale Mikoa ya jirani kupitia udhamini wetu wa mbio za Kilomita 5 za Benki ya CRDB,” amesema .



Hata hivyo, Kamati ya waandaaji wa mbio hizo imewashukuru wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Premium Lager na YAS kwa kutenga kitita cha jumla ya shilingi milioni 53 ambazo zitatolewa kama zawadi ya Mbio za kilomita 42 na kilomita 21, pamoja na vitengo vinmgine mbalimbali.

 
Waandaaji hao pia walisema kuwa tukio hilo mwaka huu,