CHUPA za plastiki kutumika kama kifungashio cha maji ya kunywa kwa matumizi ya binadamu, zimekuwa zikijadiliwa sehemu mbalimbali duniani, kuwa visababishi vya saratani.
“Hata hivyo, taarifa zilizopo kisayansi na kitafiti katika ukweli kuhusu matumizi ya plastiki kwa kufungashia vyakula na saratani, bado utafiti unaendelea,” mtaalamu anasema.
Mshauri na Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dk. Ali Mzige, alipohojiwa hivi karibuni, alifafanuzi na kutoa ushauri kwamba ni vema watu wakafuata maagizo jinsi ya kuhifadhi, kupasha na kupika chakula wanapotumia vyombo vya plastiki.
Anasema, vyombo hivyo vinaweza kutumika tena, kwa kubadilishwa endapo vimeharibika au vina matobo.
Dk. Mzige anataja baadhi ya hoja anazozipinga ni matumizi ya plastiki na uhusiano wa saratani: Kwamba maji yanapogandishwa kwenye chupa za plastiki yanaweza kuleta saratani, au kutumia kila mara plastiki nako kunasababisha ugonjwa huo.
Pia, inatajwa chupa za maji za plastiki zinapowekwa juani au kwenye gari na kupata joto, kemikali za plastiki zinapovuja kwenye vifungashio vya vyakula vinaweza kusababisha saratani.
Vilevile, kunatajwa kusababisha saratani pale unapotumia ‘microwave’ kwa kupasha chakula wakati imefunikwa na plastiki, na vifungashio vya chakula vyenye kemikali ya ‘dioxin’.
UKWELI WAKE
Dk. Mzige anasema, “ukweli wa mambo ni kwamba, chupa za maji za plastiki hutengenezwa kwa kutumia 'Polyethelene terephthalate (PET)’, kemikali ijulikanayo kama DEHA zimesingiziwa kuwa zinaweza kuleta saratani. Katika utaalamu wa kemia, uhai na maabara, kemikali hizo hazipo katika kundi la kusababisha saratani.”
Anasema, maji yapogandishwa kwenye chupa za plastki, hakuna uwezekano wa kemikali kutoka kwenye chupa ya plastiki.
Chupa za plastiki za maji zinaweza kutumika tena endapo zitaoshwa katika maji yenye vuguvugu na kutumia sabuni ya maji, ili atakayeitumia tena asipate maambukizi ya bakteria wala protozoa kama
amoeba.
Chupa ya plastiki inapoharibika au ikionyesha kuchoka, ni vema ikabadilishwa. Kwa wanaotumia vifaa vya plastiki wanashauriwa watumie vifaa vinavyoweza kutumika kwenye ‘microwave; joto lake kwenye gari haliwezi kutoa kemikali kwenye chupa za plastiki.
Akifafanua, anasema plastiki zinazotumika kufungia na kuhifadhi vyakula hutumia aina ya plastiki ‘polyvinyl chloride’ (PVC) kati ya kemikali iliyopo kwenye PVC, kemikali ya DEHA huifanya plastiki iwe laini.
Inapovuja huweza kuingia kwenye vyakula vyenye mafuta kama nyama, jibini mchakato huo huenda ukaleta madhara endapo ‘microwave’ itatumika kupasha vyakula kwenye hiyo plastiki.
ANGALIZO LAKE
Hakuna uthibitisho kuwa ‘DEHA’ inaweza kuleta saratani. Kiwango cha hizo kemikali za plastki hakijapita kiwango kilichopatikana kwenye wanyama waliofanyiwa utafiti kwenye maabara.
Anasema wanasayansi na watafiti wanashauri, binadamu achukue tahadhari, ambayo Dk. Mzige anashauri watu kutumia chombo cha plastiki kilichokubalika kutumika chenye maandishi ‘suitable for microwave’, yaani kinaweza kutumika kwenye ‘microwave.’
Na kwamba vifungashio vya maziwa ya mtindi na ‘ice cream’ haviwezi kutumika kwenye ‘microwave’. Kopo za plastiki zilivyohifadhi vipodozi anataja hazifai kuhifadhia chakula, au kugandishia maziwa.
Kuna aina ya plastiki ijulikanayo kwa jina ‘Bisphenol A’ (BPA). Plastiki hiyo ni nyeupe, inavumilia joto na haipasuki kirahisi, ndizo zinatumiwa kutengeneza chupa za maji, chupa za maziwa.
Aina hiyo ya plastiki hutumika kufungashia vyakula na vifuniko vya vyakula vya makopo.
Kemikali hiyo ‘BPA’ huenda ikaathiri mfumo wa homoni, hususan za uzazi akisema hazifai.
Pia, anataja chupa za kunyonyeshea maziwa kwa watoto zinashauriwa huko Ulaya, Canada, Uingereza na Australia na Newsealand zisiwe na kemikali ya BPA (BPA free).
Nchini Tanzania, kunashauriwa, endapo mtoto anapewa maziwa, ni vema mzazi, au mlezi atumie kikombe na kijiko, ambacho ni rahisi kukiosha na kukihifadhi.
“Tumia vifungashio vya chupa ya kioo, vyombo vya udongo wakati wa kupasha chakula.Pamoja na haya kujulikana, bado taka zinaendelea kuhusu matumizi ya chupa za plastiki katika mazingira tulio nayo,” anasema Dk. Mzige.
Anafafanua kuwa, tafiti za CDC huko Marekani, Ulaya na Australia, na CDC waliwasiliana wadau John Hopkins kuhusu uvumi kwenye mitandao wakiwanukuu dai la uthibitisho, kuwa maji kwenye chupa za plastiki yakigandishwa na yakikaa juani hayawezi kuleta saratani. Uthibitisho ulikuwa uzushi.
DIOXIN KEMIKALI HATARISHI
Dioxin ni kemikali haribifu inayosambaa angani, hewani, na kuingia kwenye maji. Kemikali hiyo ya ‘dioxin’ hutokea wakati vifaa mbalimbali na uchafu unaozalishwa kwenye viwanda au hospitalini, uchomaji masalia yakehuzalisha ‘Dioxin.’
Ng’ombe anaweza kula majani au kunywa maji yaliyochafuliwa na ‘dioxin’, kuku anaweza kulishwa chakula kilichochafuliwa na ‘dioxin’ na mayai yakapata athari.
Anasena, samaki baharini, mtoni na maziwa wanakula ‘dioxin’. Minofu yao yenye mafuta kwenye miili yao inahifadhi sumu hiyo.
Dk. Mzige, anafafanua kemikali yenye ‘dioxin’ inapopatikana kwenye nyama inayoliwa kwa muda mrefu, inakaa mwilini na kusababisha saratani za utumbo mpana na aina nyinginezo, za
kama tezi dume na saratani ya wanawake.
Anasema, katika chakula cha wanyama wanaoliwa chote kwa ujumla, akitaja asilimia 35 ya saratani zote duniani husababishwa na chakula; pia asilimia 30 ya saratani hizo, zote husababishwa na matumizi ya
tumbaku, ugoro, kuberi ndani ya tumbaku na bidhaa zake zote.
Pia, anataja ulaji matunda na mboga za majani, pia kufanya mazoezi ya mwili na viungo, husaidia kuondoa anachokitaja ‘atomi na elektroni’ haribifu mwilini.
Na kwa hali hiyo husaidia kudhibitu saratani, kisukari, shinikizo la damu na kukupa afya iliyothabitu kimwili na kiakili.
Dk. Mzige anasisitiza watu wazingatie mlo kamili wenye mchanganyiko wa virutubisho ain zote na kupunguza matumizi ya mafuta ya ziada, chumvi na sukari.
Vilevile, kupunguza matumizi yasiyo lazima ya vifaa vya plastiki kuhifadhi, kupikia na kufungashia vyakula.
Ushauri ni kuwa watu wafuate maelekezo ya watengenezaji, wafungashaji na wasindikaji vyakula vinavyoonesha kuacha kuvitumia.
• Ni ufafanuzi wake ulipotolewa. Kwa ushauri, wasiliana naye: [email protected].
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED