SAMIA ALIVYODHAMIRIA AFYA TAIFA … Amwaga mabilioni ya vituo afya 1061 na kambi uzazi hospitalini, magari wagonjwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:05 PM Jun 26 2024
Mwonekano wa upande mmoja wa jengo jipya la upanuzi wa Hospitali ya Meta jijini Mbeya, likiwa na vyumba 223, vikiwamo vitatu vya upasuaji na huduma za dharura wakati ikijengwa.
PICHA: MTANDAO.
Mwonekano wa upande mmoja wa jengo jipya la upanuzi wa Hospitali ya Meta jijini Mbeya, likiwa na vyumba 223, vikiwamo vitatu vya upasuaji na huduma za dharura wakati ikijengwa.

WAKATI sasa nchini kunatajwa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, inaimarishwa kuboresha huduma za afya nchini.

Sura ya maboresho hayo, ambayo ni sehemu ya malengo ya kiserikali hivi sasa, ni kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa, ili kupunguza rufani za wagonjwa nje ya nchi na kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi.

Vilevile, sera hiyo ambayo sehemu ya Dira ya Maendeleo Awamu ya  Sita, kunalengwa kuimarishwa mifumo ya kugharamia afya kila mwananchi anakuwa katika mfumo wa bima ya afya; kuimarisha huduma za kinga na tiba za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza; pamoja na huduma za uzazi, mama na mtoto.

Katika kurejea maono hayo ya kiafya nchini, ni maudhui ya maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akilenga katika uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya, lengo kuimarisha ubora wa huduma wa afya kwa wote. 

SURA ILIKOFIKA 2024

Hadi kufikia Machi 2024, ufafanuzi wa Wizara ya Afya umekijikita katika maeneo kadhaa, Rais Dk Samia akilenga kuguswe mustakabali wa mambok kadhaa:  

Inaanza na , kujenga miundombinu ya kutoa huduma za afya nchini, upatikanaji bidhaa za afya, ubingwa bobezi; uchunguzi wa mionzi; huduma za Afya ya Uzazi wa Mtoto.

Pia, kuna suala la magonjwa ya mlipuko; ajira kwa watumishi na udahili wa wanafunzi; Upatikanaji wa Watoa Huduma Ngazi ya Jamii (CHWs); na Sheria ya Bima ya Afya Kwa Wote. 

Aidha, Wizara ya Afya inaelekeza kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, suala la ujenzi wa miundombinu ya kutoa huduma ya afya nchini, katika Serikali ya Awamu ya Sita, kumeshafanyika uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kutoa huduma za afya.

Eneo mojawapo ni kuwapo vituo vya kutoa huduma za afya katika Serikali ya Awamu ya Sita, kumeongezeka kutoka 8,549 mwaka 2021 hadi kufikia 9,610 Machi 2024; ikiwa ni ongezeko la vituo 1,061.

Sambamba na hilo, inafafanuliwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita,  kumefanyika uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kutoa huduma za afya, vikiongezeka kutoka vituo 8,549 mwaka 2021 kufikia vituo 9,610 Machi 2024.

Hapo ni sawa na ongezeko la vituo 1,061, inayojumuisha zahanati; vituo vya afya; hospitali zenye hadhi za wilaya na rufani ngazi ya mkoa na kanda; hospitali maalum na taifa.

UWEKEZAJI MKUBWA UZAZI

Eneo lingine linatajwa kujumuisha suala la kuimarisha huduma za Afya, Uzazi, Mama na Mtoto unaochukua nafasi katika sura ya uwekezaji mkubwa wa mfano, unaojumuisha: Kukamilishwa ujenzi wa jengo la kutoa huduma za afya ya Mama na Mtoto – Hospitali ya Meta, iliyopo jijini Mbeya kwa thamani  shilingi 13.2.

Lingine linatajwa ni uendelezaji wa majengo ya huduma za Mama na Mtoto kwenye Hospitali za Rufani Sekou Toure jijini Mwanza; pia miradi mikubwa  katika hospitali za Geita, Simiyu, Mawenzi (Moshi), Njombe na Songwe, zikigharimu shilingi bilioni 71.1. 

UPATIKAAJI HUDUMA

Taarifa ya Wizara ya Afya, inafafanua kumeimarishwa sasa upatikanaji wa bidhaa za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ndani ya miaka mitatu sasa, ikipatikana katika vituo vinavyomilikiwa na serikali, umeongezeka kutoka asilimia 82.5 mwaka 2021 hadi asilimia 88.2

mwaka 2023.

Lingine ni suala la kuimarishwa huduma za saratani ya mlango wa kizazi, kukiwapo jumla ya mashine 140 za uchunguzi wa saratani zimenunuliwa na kusambazwa kwenye vituo 140, vya kutoa huduma za afya katika

Halmashauri 104, ndani ya mikoa 26, jumla ya vikiwa na thamani ya shilingi bilioni 1.1.

UPASUAJI WAJAWAZITO 

Eneo lingine katika orodha hiyo ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita, ni kwamba kumeimarishwa huduma za upasuaji wajawazito kwa kuongeza vituo vyenye uwezo kwenye huduma za upasuaji wadharura, kumtoa mtoto tumboni kutoka vituo 340 kitaifa vya mwaka 2021 hadi kufikia 523 mwaka 2023.

Mustakabali mwingine ni kuanzishwa wodi maalum kwa ajili ya kuhudumia za watoto wachanga wagonjwa, hadi kufika Disemba mwaka jana, zilikuwa jumla ya hospitali 189 zinazohudumia, ikilinganishwa na 165 mwaka 2022 na mwaka 2018, zilikuwapo 14 pekee.

Hapo kukaendana na kuimarishwa upatikanaji bidhaa za afya ya uzazi, mama na mtoto katika vituo vinavyomilikiwa na serikali, umeongezeka kutoka asilimia 82.5 mwaka 2021 hadi asilimia 88.2 mwaka 2023.

SARATANI MLANGO KIZAZI

Ripoti hiyo ya kiserikali inafafanua kwamba, kumeimarishwa huduma za saratani ya mlango wa kizazi, kwa kuwapo mashine 140 za uchunguzi wake, zikinunuliwa na kusambazwa kwenye vituo 140 vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri 104 ndani ya mikoa 26. Jmla ya vufa hivyo vina thamani ya shilingi bilioni 1.1

MFUMO M-MAMA

Mfumo wa huduma za dharura wa kieletroniki unaoitwa kitaalamu ’M-mama’, unaoratibu rufani, kwa kusafirisha kinamama wajawazito na watoto wachanga wanaohitaji huduma za dharura, inafafanuliwa Serikali ya Awamu ya Sita, imeshauanzisha hadi kwenye vituo vya afya inatajwa  kati ya mwaka 2022 hadi mwaka 2023, mfumo huu umeendelea kufanya kazi katika mikoa yote 31 Tanzania Bara na Zanzibar, kukiwapo mageuzi makubwa ya kuhudumia Watoto wachanga.   . 

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akiwa katika wodi maalum ya kuhudumia watoto wachanga wagonjwa katika Hospitali ya Rufani Mount Meru Mkoani Arusha, akashuhudia mfumo huo unavyorahisisha utoaji wa huduma za dharura kwa wakati.

KUJIFUNGULIA HOSPITALINI

Kuna suala la kuongezeka wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya afya kutoa huduma za afya, nchini, idai imeongezeka maradufu, kutoka asilimia 63 mwaka 2021 hadi asilimia 85 mwaka jana.

“Lengo la nchi ni kufikia asilimia 95 ya wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ifikapo mwaka 2030,” inafafanua taarifa yua Wizara.

MAGARI YA WAGONJWA

Suala la kuwapo magari ya kubebea wagonjwa yanunuliwa na kusambazwa kila kona na Rais Dk. Samia, ameshakabidhi jumla yao 216, kwa ajili ya kurahisisha utoaji matibabu ya dharura.

Hiyo imeendana na serikali kununua jumla ya magari ya kubebea wagonjwa 727, yakienda kusaidia usafirishaji wagonjwa, wakiwamo kinamama wenye changamoto za uzazi kwa haraka na kuwafikisha katika huduma za rufani, hivyo kupunguza adha kwa wananchi, sambamba na kuepuka vifo vinavyozuilika.