Afrika Kusini yaunda Baraza la Mawaziri, ANC bado kinara

By Ani Jozeni , Nipashe
Published at 12:24 PM Jul 03 2024
Kiongozi wa DA, John Steenhuisen, akipongezana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Vyama vyao vimeunda serikali ya mseto.
PICHA: MTANDAO
Kiongozi wa DA, John Steenhuisen, akipongezana na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Vyama vyao vimeunda serikali ya mseto.

RAIS Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameunda Baraza la Mawaziri, licha ya jina na Waziri wa Kilimo kutotolewa mapema, ila atatokana na Chama cha Democratic Alliance (DA). Wateule wengi wanatokea African National Congress (ANC).

Wizaya za Fedha na Viwanda Nishati, Usafirishaji na maeneo yamayohitaji mageuzi, mengi yamebakia ANC.

Wakati ambapo sera za umiliki ardhi hazihitaji mabadiliko ila  wakulima wa Kizungu wanahitaji, nje ya maeneo ya jadi ya Wazulu na makabila makubwa kadhaa, ni eneo hilo ambalo DA ilipewa kama wizara yake muhimu ya kwanza. 

Cha kushangaza ni kuwa hata wakati Rais Ramaphosa anaitoa orodha ya Baraza la Mawaziri nafasi ya Waziri wa Kilimo ilikuwa haijajazwa, hali inayoashiria kuwa waziri atatoka DA lakini apatikane mtu ambaye ANC wanamkubali. 

Suala la mashamba au kilimo linaweza kuwa nyeti mbele ya safari, hivyo anatakuwa waziri ambaye hatazusha matatizo na wanaharakati ANC au makundi yaliyojitoa ANC na kuunda upinzani.

Hizo ndiyo habari mpya baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Bunge la Afrika Kusini na chama tawala cha ANC kupata chini ya asilimia 42 ya kura. Hali iliyosababisha iundwe serikali ya mseto ili kuwa na wingi wa viti bungeni. 

Ramaphosa hakuchukua muda kujiweka tayari kwa hatua hiyo, ila mjadala wa ndani ya ANC kuhusu serikali ya mseto sasa umetoa hitimisho. 

Ni serikali ya ANC ambako wapo wahusika wa vyama kadhaa na  chama kikubwa ni DA. Hakuna ushirikiano wa kiitikadi ambako masuala ya fedha, biashara yanashikwa na DA huku ulinzi, mambo ya nchi yapo ANC. Nyakati za Nelson Mandela akiwa rais, Inkatha Freedom Party (IFP),  ilikuwa na Wizara ya Mambo ya Ndani na kukaimu urais kama Mandela na Naibu Thabo Mbeki wamesafiri. Ilijenga umoja wao kitaifa na kuondoa vurugu za makundi ya Wazulu walioona wananyanyaswa na ANC.

ANC imerudi katika mfumo wa awali kwa kushirikiana an DA, chama cha naibu wa kwanza wa Mandela, Frederick de Klerk, ambaye aliwaongoza Wazungu walio wachache kukubali utawala walao wengi. Mkataba wa ANC na IFP kuungana na DA ndiyo tangu mwanzo ulikuwa unaonekana kuunda serikali yenye tija, si ya malumbano na kuharakati kama Chama cha Jacob Zuma cha Umkhonto we Sizwe ukimaanisha mkuki wa taifa,  au cha Julius Malema cha EFF kinachozungumzia  kutaifisha mali za Wazungu.

Serikali thabiti kisera ni muungano wa ANC na DA, na IFP cha Wazulu  wahafidhina hivyo wanaendana na DA, tofauti na MK  au EFF. Wako waliotaka serikali ya umoja wa kizalendo lakini isingetatua lolote katika mikwamo ya uchumi na kijamii inayovuruga imani ya wapigakura kwa ANC.

 Kwa vile ndiyo chama katika uundaji serikali,  ANC inatakiwa itumie nafasi ya kuunda umoja wa kitaifa, kusikiliza hoja za mageuzi na kuzifanyika kazi, na siyo kubaki katika dhana kuwa hawa wa DA na IFP wamekuja tu kutafuta vyeo.

Ina maana kuwa nje ya hapa kila kitu kinawezekana, pamoja na kuwa ukiangalia hali ya kiuchumi na kisiasa nchini humo, kila aina ya mseto  itakuwa na majaribu ya aina moja au nyingine kiitikadi na kisiasa, iwe ni kwa chama cha ANC chenyewe au ni kwa Rais Ramaphosa kama kiongozi. 

Moja ya maeneo hayo ni kuungana na Democratic Alliance kama jumuia ya wafanyabiashara na kwa jumla wanadiplomasia wa Ulaya na Marekani wanavyotaka, huku wale wa Afrika ni kama wanaangalia tu. Ila kwa nchi iliyozoea utawala wa uelekeo wa kimapinduzi, ANC ni wale watakaokufua biashara.

Ina maana kuwa kupata muunganiko wa kiitikadi unaoiinua ANC na Afrika Kusini mbele ya macho ya dunia inabidi chama hicho kihame kutoka uasili wake na kurudi katika mwenendo wa mageuzi iliyoukataa kwa takriban miaka 25 tangu demokrasia halisi ipatikane.

 Mwelekeo huo ulikuwa thabiti ukisimamiwa na Rais Mandela, aliyeacha uelekeo wa kiharakati au hata kimapinduzi kutokana na mwanga kuhusu amani na maridhiano ulioasisiwa na Askofu Desmond Tutu. Mrithi wa Mandela, Thabo Mbeki, alikwama kusititiza mwelekeo huo, itikadi ya harakati ikachukua nafasi yake, pamoja na udhaifu mwingine kwa mfano kutawala raslimali zote.

Lakini utawala wa Jacob Zuma, uliiasi  ANC kutokana na mashauri ya kisheria kumepunguza kwa nguvu kura ANC, na baadhi watataka kuwepo na maridhiano na kundi la kiongozi huyo, aombwe radhi....