Zitto awakumbuka wapigania mageuzi ya vyama vingi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:05 PM Sep 16 2024
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Picha:Mpigapicha Wetu
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe

Katika kusherehekea Siku ya Demokrasia Duniani Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema wakati nchi nyingine wanasherehekea siku ya demokrasia Tanzania bado inajikongoja kuelekea demokrasia.

Katika mkutano aliofanya mkoani Njombe katika Jimbo la Lupembe jana Septemba 15, 2024 Zitto alisema; "Tunawakumbuka na kuwapa heshima wote waliopigania Demokrasia ya Nchi yetu, waliotangulia mbele za haki na walio hai. Kina Maalim Seif, Kina Shaaban Mlowo, kina Bob Makani, kina Jenerali Ulimwengu, kina Marando, kina James Mbatia, kina Freeman Mbowe, kina Msafiri Mtemelwa na wengine wote"

Zitto ameongeza kuwa Demokrasia ndio msingi wa maendeleo, huku akieleza kuwa ACT inaamini demokrasia inachochea maendeleo.

Zitto Kabwe anaendelea na ziara ya awamu ya pili ya kuyafikia majimbo 214 katika mikoa 26 ya Tanzania bara ambapo yeye anaendelea na ziara Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.