Waziri Lukuvi, atembelea Mradi wa Ujenzi wa Mfereji Mkombozi, Pawaga

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:20 PM Oct 01 2024
Waziri Lukuvi, atembelea Mradi wa Ujenzi wa Mfereji Mkombozi, Pawaga
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri Lukuvi, atembelea Mradi wa Ujenzi wa Mfereji Mkombozi, Pawaga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi, Mbunge wa Isimani amesema Mfereji Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mkombozi unaojengwa na Serikali katika Bonde la Pwaga utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kujishughulisha na kazi za kilimo.

Waziri ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo na kufanya Mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Mbuyuni, Kimande, Itunundu, Mbugani, Mboliboli katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa jana.

Uwekezaji unaofanya na serikali utasaidia kuwainua wananchi wengi kiuchumi kwa kuwa na maisha bora zaidi kwa mashamba wanayolima lakini kwa mashamba mengine mapya hekari 15,000.

“Tunamponge sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa wa uchumi wa Mkoa wa Iringa na kwa Bonde la Pawaga,” alisema Waziri Lukuvi.

Tunaamini Mkandarasi utautekeleza Mradi wa ujenzi kwa ufanisi mkubwa, na Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha fedha za mradi zinapatikana ili mradi huo wa umwagiliaji ulio mkubwa kuliko miradi mingine yeyote ya umwagiliaji ukamilike kwa wakati.

Kwa Upande wake Mhandisi wa Ujenzi wa Mfereji wa umwagiliaji Abdulhamid Mbaba kutoka Comfix and Engineering Limited amesema mradi bado upo kwenye hatua za utekelezaji kwa kuhusanisha ujenzi wa miundo mbalimbali kama Ujenzi wa Banio, Ujenzi wa Mfereji Mkuu, Ujenzi wa Barabara na Ujenzi wa Vigawa Maji  kwa Lot namba 1.

Ujenzi wa Lot namba 2 unahusisha Ujenzi wa Mfereji Mkuu wenye Urefu wa Km 16.1, Ujenzi wa Tuta la kuzuia Mafuriko na Barabara na Ujenzi wa Vigawa Maji.

Mhandisi Mbaba alisema, “Ujenzi wa Lot namba 1 Ujenzi wa banio umekamilika kwa 98%, Ujenzi wa Mfereji Mkuu na Kichuja Mchanga umekamilika kwa 50% huku Ujenzi wa Barabara ukikamilika kwa 95%”
Aidha kwa Lot namba 2 Ujenzi wa Mfereji Mkuu na Kichujio Mchanga umetekelezwa kwa 36% Ujenzi wa Kichujio Mchanga na barabara umefikia 62%.

7