Watano wapandishwa kizimbani tuhuma wizi vifaa vya umeme vya Sh. milioni 54

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 06:02 PM Sep 12 2024
Watano wapandishwa kizimbani tuhuma wizi vifaa vya umeme vya Sh. milioni 54
Picha: Shaban Njia
Watano wapandishwa kizimbani tuhuma wizi vifaa vya umeme vya Sh. milioni 54

WATU watano umepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kahama kwa tuhuma za wizi wa nyaya za umeme aina ya Aluminium zenye thamani ya Sh.milioni 54 zilizokuwa zinatarajia kutumika katika mradi wa usambazaji wa Nishati ya Umeme Vijijini kata ya Idahina Halmashauri ya Ushetu.

Wakisomewa mashtaka hayo na Mkuu wa Mashtaka Ofisi ya Kahama,Jukaeli Jairo aliiambia mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 3 mwaka huu katika miji ya Kahama na Dar es Salaam ambapo walikutwa na gram tatu za nyaya huo.

Jairo amesema, watu hao wanakabiliwa na makosa mawili, kosa la kwanza ni kuunda genge la uharibu kwa makusudi kinyume na sheria 4(1) (a) iliyosomwa na sheria namba 57(1) na 60(2) ya sheria ya uhuju uchumi, huko kosa la pili likiwa ni wizi kinyume na kifungu cha sheria namba 258(1)(2)(a) na 265 ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Aidha aliwataja watu hao kuwa ni ; Erick Kamuhanda Rweyemamu(36), Kaijage Kagenyi(27),Carlos Eck Chamanga(29), Ngwea Mkomwa Sufian(29), Lemi Paul Mtwale(34) wote wakiwa ni mafundi umeme pamoja na Rotan Eliezer Nzowa(38) Mkandarasi wa umeme.

1

Kesi hiyo yenye namba 26208/2024 ilisililizwa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa Wilaya ya Kahama Edmund Kente na mzigo uliyoibwa ilikuwa mali ya Iddcon Investment Limited aliyekuwa akitekeleza mradi wa REA katika Kata ya Idahina Halmashauri ya Ushetu.

Watuhumiwa wote waliomba Mahakama kupata dhamana lakini hakimu Kente aliwaeleza kuwa hajapata kibali cha kusikiliza shauri hilo kwasababu kosa la kwanza ni Uhujumu Uchumi na mahakama yake haina uwezo kusikiliza na kuahilisha kesi mpaka Septemba 27 mwaka huu.