Wanawake 3,000 Singida kushiriki Tamasha la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 04:09 PM Oct 07 2024
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.
Picha: Thobias Mwanakatwe
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.

MKOA wa Singida umeandaa tamasha kubwa litakalo washirikisha wanawake zaidi ya 3,000 kutoka wilaya zote za mkoa huu lililobeba jina la Wanawake na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akizungumza leo Oktoba 7, 2024 na waandishi wa habari, amesema tamasha hilo litafanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye viwanja vya Bombadia vilivyopo Manispaa ya Singida.

Amesema Spika wa Bunge mstaafu ambaye pia ni Kamisaa wa Sensa nchini, Anne Makinda, atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lengo lake ni kuwahamashisha wanawake  kushiriki katika uchahuzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.

"Serikali yetu bora na sikivu chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, imeweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata taarifa sahihi za uchaguzi na anahamasishwa ili aweze kushiriki katika uchaguzi na hivyo kutimiza haki yao ya kikatiba, hivyo tamasha hili ni moja ya mipango ya mkoa katika kuwafikia wananchi wengi hasa makundi maalum ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu," amesema Dendego.