UKATILI na udhalilishaji wa kingono katika Mkoa wa Kilimanjaro, hivi sasa sio jambo la aibu tena, baada ya kanzidata ya Jeshi la Polisi, kuonyesha kuna makosa 68 yameripotiwa.
Eneo lenye makosa mengi ya ukatili wa kijinsia, ni ubakaji ambalo lina kesi 42, likifuatiwa na ulawiti, lenye kesi 18.
Taarifa ya mwaka ya Jeshi la Polisi, mkoani humo, iliyotolewa leo Desemba 31, 2024 na Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Simon Maigwa, inaeleza kuwa makosa hayo ni tishio kati ya kipindi cha Januari hadi Disemba 2024.
Makosa mengine yaliyoripotiwa, ni makosa manne ya kuwapa mimba wanafunzi, na ukatili dhidi ya watoto manne, hivyo kufanya jumla ya makosa kuwa 68.
Kwa mujibu wa SACP Maigwa, kati ya makosa hayo ya ukatili wa kijinsia, washtakiwa wote katika kesi hizo wamepewa adhabu ya kifungo cha maisha na miaka 30 jela.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED