Serikali yaombwa kuajiri walemavu

By Peter Mkwavila , Nipashe
Published at 03:17 PM Apr 25 2024
Serikali yaombwa kuajiri watu walemavu.
PICHA: MAKTABA
Serikali yaombwa kuajiri watu walemavu.

SERIKALI imeombwa kutoa asilimia tatu ya ajira ilizotangaza kwa makundi ya watu wenye ulemavu katika sekta ya elimu na afya ili kukabiliana na uhaba wa watumishi nchini.

Hivi karibuni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Geore Simbachawene alitangaza ajira mpya zaidi ya 46,000 kwa watumishi wa sekta ya afya wapatao 12,000 na elimu10,000. 

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Karakana ya kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu mkoani hapa, Mwita Marwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa baada ya kutangazwa ajira hizo.

Marwa, amesema serikali ikitimiza maelekezo hayo ya kutoa ajira kwa asilimia tatu kwa makundi hayo, itawaondolea adha kupita ofisini na vyeti vyao kuomba kazi.

"Wengi wao wamekuwa wakitembea maofisini na vyeti kwenye mikoba hadi vinachakaa , tunaiomba serikali kwa nafasi hizo wasisaulike," amesema.