Rais Samia awasili China kushiriki mkutano wa FOCAC

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:35 PM Sep 03 2024
Rais Samia awasili China kushiriki mkutano wa FOCAC
Picha: Ikulu
Rais Samia awasili China kushiriki mkutano wa FOCAC

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wakuu wa nchi za Afrika na China mkutano huo unaotarajiwa kuaanza Septemba 4 hadi 6 mwaka huu nchini China.

Atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Rais Samia atahutubia ufunguzi wa mkutano wa FOCAC.

Aidha, Rais Samia atafanya mazungumzo na Rais China,  Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa hati za makubaliano ya uboreshaji wa reli ya Tazara.

Pia Rais atakutana na makampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.