Polisi Monduli watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalum

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:13 PM Sep 16 2024
Polisi Monduli watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalum
Picha: Polisi Monduli
Polisi Monduli watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalum

Askari Polisi Wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wilayani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Radegunda Marandu, wametoa msaada wa nguo na vyakula mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji maalum wilayani humo.

Msaada huo ulitolewa mapema jana katika Kituo cha Walemavu cha Saint John Paul II Rehabilitation Centre kilichopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuihudumia jamii kuelekea kilele  cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Polisi wilayani humo SSP. Radegunda Marandu, alisema kwamba, wamefanya hivyo ili kuliweka kundi hilo karibu hali ambayo itasaidia kushirikishana mambo mbalimbali ikiwemo kupeana taarifa za uhalifu.