TAKRIBANI simu 120 zimekamatwa shuleni, huku zilizo nyingi zikiwa na maudhui yanayohusu ngono na uhusiano kimapenzi.
Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Tabora, Nestory Mashiku, ameyasema hayo mkoani humo, na kwamba wamebaini hilo baada ya wanafunzi kukutwa na simu janja shuleni.
“Tunaziona simu kama nyenzo ya kufundishia ila ni kama inaharibu watoto wetu. Mtoto ana utaalamu wa kutumia simu kuliko mzazi wake. Nilikuwa katika kikao shuleni fulani nimeshuhudia simu zaidi ya 120 zilikusnaywa, wana makundi na wanasambaza taarifa.
Baadhi simu zina picha za ngono na wana-share (wanasambaza), wametengeneza na kundi, ila wengine katika simu zao wana uhusiano, wanapeana taarifa tukutane saa ngapi? Hali sio salama, kila mmoja afanye kazi yake, ulinzi na usalama wa mtoto ni wajibu wetu,” amesema Mashiku.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED