Mwanafunzi afariki kwa kugongwa na gari, wananchi wafunga barabara

By Ida Mushi , Nipashe
Published at 06:47 PM Oct 24 2024
Ajali Morogoro
Picha:Ida Mushi
Ajali Morogoro

WANANCHI wa Kijiji cha Tabu Hotel wamefunga barabara kuu ya Dodoma-Morogoro tangu majira ya saa 11 wakishinikiza kufika Mkuu wa Mkoa wa Morogoro bwana Adam Malima baada ya gari ya serikali aina ya Cruzer kumgonga mwanafunzi kwenye kivuko cha watembea kwa miguu na kusababisha kifo chake na gari husika kukimbia.

Wanasema hawataki alama peke yake wanataka matuta kwasababu ajali eneo hilo zimekuwa za mara kwa mara zikihusisha magari ya Serikali zikiua wananchi wakiwemo wanafunzi.