Mikoa ya Singida-Simiyu-Arusha kuunganishwa na barabara ya lami

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:27 AM Oct 24 2024
Mikoa ya Singida-Simiyu-Arusha kuunganishwa na barabara ya lami
Picha:Mpigapicha Wetu
Mikoa ya Singida-Simiyu-Arusha kuunganishwa na barabara ya lami

Wakazi wa Wilaya ya Iramba na Mkalama, mkoani Singida, wanatarajia kunufaika na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami itakayounganisha mikoa ya Singida, Simiyu, hadi Arusha.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, ametembelea na kukagua barabara hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 65.

Silaa amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo unaoonesha namna Serikali inavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake.

Awali, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Singida, Msama Msama, ameeleza kuwa kipande cha barabara kinachojengwa kati ya Kitukutu-Gumanga-Mkalama na Chemchem-Sibiti, kikiwamo Kitukutu-Kinampanda, chenye urefu wa kilomita 7.7, kitagharimu Sh.bilioni 9.31 na kinajengwa na mkandarasi mzawa.