HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, imeanzisha kliniki mbili ikiwamo ya miguu, ili kubaini uwapo wa ganzi na presha miguuni.
Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam MNH-Mloganzila, ambaye pia ni Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Kisukari na Homoni, Dk. Faraja Chiwanga, alisema hayo leo, Novemba 14, 2024, Dar es Salaam, kwenye maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani.
Amesema kwamba kati ya athari zinazowakumba wanaougua ugonjwa huo ni kuviathiri viungo vvya mwili kama vile miguu huku baadhi ya wanaume wakikosa nguvu za kiume na wanawake kukosa hisia za kushiriki tendo, hivyo kliniki hiyo mpya itabaini dalili za tatizo mapema.
“Kuanzishwa kwa huduma hizo hospitalini hapa ni mwendelezo wa serikali wa kuboresha huduma za afya nchini, ikiwamo kuanzisha matibabu ya ubingwa bobezi ambayo hayapatikani hapa nchini, kuwapunguzia usumbufu wananchi na gharama za kutafuta huduma hizo nje ya nchi."
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED