Mbunge Ikupa aahidi kuendelea kuwatetea wenye ulemavu bungeni

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 06:57 PM Aug 12 2024
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)kundi la Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa.
Picha: Mpigapicha Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)kundi la Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa.

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)kundi la Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amesema ataendelea kuzisemea na kutetea changamoto za watu wenye ulemavu ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.

Ikupa ametoa kauli hiyo leo kwenye kongamano lililowashirikisha watu wenye ulemavu, wadau wa maendeleo na madiwani kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

Ikupa amesema kama mwakilishi wa kundi la watu wenye ulemavu bungeni, amekuwa mstari wa mbele kuzisemea changamoto za kundi hilo na kwamba anafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuzitatua.

Ametolea mfano tatizo la uchache wa walimu wenye taaluma na uwezo wa kufundisha kundi hilo na kwamba tayari  serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha vyuo vinafundisha lugha ya alama na elimu ya  wenye uhitaji maalumu.

1

"Kwa hiyo msione kama hakuna kinachofanyika, serikali imesikia maombi yetu na inayafanyia kazi, muda si mrefu tutakuwa na wataalamu wa kutosha wa kufundisha kundi hili, tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulifanyia kazi hili,"amesema Ikupa.

"Si kwenye elimu pekee lakini pia na kwenye sekta mbalimbali nako serikali imetusikia inafanyika kazi ikiwamo sekta ya afya, kwa hiyo tushukuru kwa hatua hizi zinazochukuliwa na serikali tunaamini itaendelea kufanyia kazi changamoto zetu zote tuwe wavumilivu."

Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili namna watu wenye ulemavu wanavyoweza kuingia kwenye fursa mbalimbali za kiuchumi na kisiasa.

2