MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamegoma kujadili na kupitisha Bajeti ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), kwa madai kuwa haikupelekwa na kujadiliwa na kwenye vikao vya awali.
Aidha, wamedai kuwa hawajalipwa stahiki zao zaidi ya Sh. milioni 5 kwenye kikao cha bajeti kilichofanyika Aprili mwaka huu.
Kukokana na madai hayo madiwani hao waligoma kupokea na kujadili taarifa ya TARURA na kumtaka mwakilishi kutoka nje.
Hayo yalijitokeza leo Oktoba 3, 2024 wakati wa kikao cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024/2025 cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Chiwana Said Makunganya, Said Kiosa na Mbale Motta wa Kata ya Kalulu pamoja na mambo mengine wamesema hwapati ushirikiano wa kutoka kutoka TARURA.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Hairu Hemedi Mussa, amesema ushirikiano kwa madiwani hao umekuwa mdogo jambo linalokwamisha kazi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED