Kamati yaridhishwa utekelezaji ujenzi shule ya Shimbo

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 07:46 PM Sep 12 2024
Kamati yaridhishwa utekelezaji ujenzi shule ya Shimbo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kamati yaridhishwa utekelezaji ujenzi shule ya Shimbo.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Wizara ya Elimu na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeridhika na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Shimbo iliyopo Kata ya Mkuza,Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Husna Sekiboko  amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.Samia Suluhu Hassan ndoto na maono yake ni kuhakikisha watoto wa wanapata elimu bora  kwenye mazingira rafiki ili kuandaa wataalamu wa kulitumikia Taifa lao.

Amesema kwamba Kibaha Mji wamesimamia Ujenzi wa shule hiyo kwa viwango na thamani ya fedha iimeonekana.

Pia Mwenyekiti wa Kamati hiyo ametoa maelekezo ya kamati kuhakikisha Shule zote nchini kuwa na utaratibu wa kukagua maudhui ya vitabu kama vinaendana na maadili ya Watanzania, pia vitabu hivyo vihakikiwe na kugongwa mihuri wa kuridhia matumizi na Kamishina wa Elimu nchini

Maelekezo mengine ni ,Serikali kuangalia upya mgawanyo wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi kwani yapo maeneo wanakamilisha Ujenzi na maeneo mengine hawakamilishi ama Kujenga chini ya Kiwango na kuathiri matarajio na malengo.

1

Ameitaka Wizara ya Elimu kufanya tathmini ya kimaeneo ili fedha zinazotolewa zitosheleze ili kuongeza tija ya Miradi husika

Sambamba na maelekezo hayo  amempongeza  Dk.Rogers Shemwelekwa Mkurugenzi wa Mji Kibaha kwa usimamizi wa Miradi ya Maendeleo kwa kushirikiana na Baraza la Madiwani ambao wamehakikisha fedha zinazotolewa na Serikal zinafanyakazi  na kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji ameieleza Kamati hiyo kuwa Shilingi milioni 528,998,425 kupitia Mradi wa SEQUIP zimepokelewa kwa  ajili ya Ujenzi wa miundombinu  27  na tayari imekamilika.
2
Amesema tayari Wanafunzi 281 kati yao wavulana 149 na Wasichana 132 wameanza kutumia majengo hayo na kuwapunguzia umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 8 kuifuata shule Mama ya Nyumbu.

Naye Hamisi  Taletale ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa Mradi na kushauri kujengwa kwa uzio ili kuwawekea utulivu wanafunzi wakati wa Masomo.

Waziri wa Elimu Prof.Adolf Mkenda ameishukuru Kamati kwa kazi nzuri na kupokea maelekezo yote  ya Kamati kwa ajili ya kufanyia kazi.