Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesisitiza kuwa masuala ya utekaji na kupokea kwa watu hayapaswi kufumbiwa macho.
Amesema ..."Hakuna watu wasiojulikana, kuna kundi linakamata watu, linaua watu na kuwatesa kwasababu wanazojua wao, vyombo vya ulinzi na usalama vimeshindwa kutupa majibu ya kinagaubaga"
Kiongozi huyo ameendelea kusema kuwa "Tunataka majibu, Tunataka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji kuchunguza matukio haya kisha itoe majibu kwa wananchi"
Kiongozi huyo ameyasema hayo Jana tarehe 11 Septemba 2024 Katika Jimbo la Kibaha vijijini. Semu anaendelea na ziara ya awamu ya pili ya kuyafukia majimbo yote 214 ya Tanzania bara.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED