KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesisitiza amani, umoja na mshikamano na kwamba ndio kitu cha thamani tulichonacho Watanzania na kuwa ni lazima tulinde kwa wivu mkubwa.
Nchimbi ameyasema hayo Bariadi mkoani Simiyu, alipoongea na wananchi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake inatofanyika katika mkoa huo na Shinyanga.
“Umoja wa taifa letu nitaendelea kusisitiza kila nitakapokuwepo kwamba umoja na mshikamano wa nchi yetu ndio kitu cha thamani tulichonacho kuliko kitu kingine chochote, watanzania lazima tulinde kwa wivu mkubwa.
“Watanzania wa vyama vyote tunapaswa tujue jambo ambalo tulilonalo lenye thamani kubwa ni amani, umoja, mshikamano wa taifa letu.” amsema Nchimbi
Dk. Nchimbi ameongeza kuwa: “Na kila anayejaribu kuuvuruga umoja huu tumwambie kwa macho makavu kwamba hatua tayari kuvumia kuipeleka nchi yetu katika machafuko.” ameonya
Akizungumzia miradi mikubwa ya maendeleo iliyofanikiwa ikiwemo mradi wa reli ya kisasa (SGR), Mradi wa kufua umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere
Hakuna mtu aliyeamini kwamba baada ya kuondoa Rais wetu mpendwa Magufuli basi miradi ile ingekamilika hakuna mtu aliyeamini.
Amesema mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere umebakiza asilimia 1 na kidogo kukamilika huku ule wa reli ya kisasa imefika Dodoma na inafanyakazi.
“Mapigo ambayo Rais Samia ameyafanya sio madogo, na hata aliyoyaeleza mbunge wenu Enginner (Andrea) Kudo yote yanaonesha uwezo wake mkubwa (Rais samia) wa kutenda kazi lakini pia mapenzi kwa wananchi wake.”
Amesema Rais Samia ameonesha kwa vitendo kuwa anapenda watu wake kwa kuhangaika kutafuta fedha za miradi ya maendeleo na kusimamia kuhakikisha inatekelezwa.
“Tunapenda na tunataka kuwa na Rais ambaye anaweza kuonyesha kwa vitendo kwamba anapenda watu wake, Rais Samia ameweza kuonyesha kwa vitendo kwamba anapenda watu wake kwa jinsi anavyo hangaika kutafuta fedha za miradi ya maendeleo lakini anavyohangaika kuisimamia na kuhakikisha inatekelezwa.
“Kwa hiyo kazi tuliyonayo ni ya kuendelea kumuunga mkono ili aendelee kuitumikia nchi yetu kwa uaminifu, upendo mkubwa na nchi yetu iendelee kupata maendeleo.” amesema Nchimbi
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED