ACT Wazalendo wataka vituo vya kusambazia gesi

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 01:37 PM Jul 01 2024
Naibu Waziri Kivuli wa Fedha wa chama hicho Shangwe Ayo.
Picha: Sabato Kasika
Naibu Waziri Kivuli wa Fedha wa chama hicho Shangwe Ayo.

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka serikali kuongeza vituo vingi zaidi kwa ajili ya kusambazia gesi ili kuendeleza sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Kivuli wa Fedha wa chama hicho Shangwe Ayo na kufafanua kuwa ni vyema pia kuwapo miundombinu ya upatikanaji wa gesi asilia kwa urahisi.

"Kwa Sasa Kuna vituo vitano tu, ni vyema serikali ijenge vingine zaidi nchi nzima, ili kusogeza huduma karibu na wananchi, kwani uagizwaji wa mafuta wa hutumia dola za Kimerakani lakini bei inapopanda huwa ni tatizo, hivyo ni vyema serikali ikawekeza kwenye gasi asilia," amesema Shangwe.

Aidha, waziri kivuli huyo amesema, hatua ya serikali ya kuondoa tozo ya shilingi 383 katika kila kilo ya gesi ni nzuri, kwa kuwa tozo hiyo ingeenda kuua matumizi ya gesi asilia kwenye vyombo vya moto.

"ACT Wazalendo tunaendelea kusisitiza kwamba ili kupunguza matumizi ya serikali kuna ulazima wa magari yote ya serikali na mwend 10o kasi kufunga mitambo ya gesi," amesema Shangwe.

Amesema, kuanzia Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, serikali imetumia takriban Sh. trilioni 7.7 kuagiza mafuta na kwamba kiasi hicho kingepungua kama matumizi ya gesi yangekuwa makubwa.

"Hivyo serikali ijenge vituo vingi zaidi vya kujazia gesi katika maeno mbalimbali nchini, badala ya kutegemwa vitano vilivyopo," amesema.