Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amekagua mradi mkubwa wa maji na uchimbaji wa visima virefu vya maji katika Wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha.
Mradi huo mkubwa wa maji unatekelezwa baina ya Tanzania na Dubai inayoongozwa na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai na makamu wa Rais wa milki za kiarabu (UAE) ukiwa na malengo ya kuchimba visima virefu 37.
"Leo tunakuja kuwaambia kuwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Mwanadiplomasia namba moja, Mkuu wa nchi yetu na Rais wetu ametujengea mahusiano mazuri na nchi za Falme za kiarabu na sisi wana Ngorongoro tumeanza kuyaona matunda hayo ikiwa ni ndoto na shauku ya Makamu wa Rais Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.", amesema Makonda.
Makonda amesema hadi sasa jumla ya visima 18 vimeshachimbwa kwenye vijiji mbalimbali na 12 vimeshakamilika na wananchi wameanza kunufaika na huduma ya maji.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED